Tundu Lissu Kusafirishwa Nje ya Nchi kwa Matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tundu Lissu Kusafirishwa Nje ya Nchi kwa Matibabu
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu sasa imezidi kuimarika na kusema atasafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Mbowe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya chama hicho, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya Tundu Lissu na kusema mpaka sasa Mbunge huyo anaendelea vizuri na kudai amefanyiwa upasuaji mara 17.
"Tundu Lissu mpaka sasa amefanyiwa upasuaji mara 17 amewekewa damu nyingi kuliko mgonjwa yoyote katika hospitali ya Nairobi lakini Mungu ameendelea kutenda miujiza kwake, saizi mashine zote zilizokuwa zinamsaidia zimeondolewa, saizi hapumulii mashine tena, mirija yote aliyokuwa anatumia kwa ajili ya chakula imeondolewa na juzi kwa mara ya kwanza aliweza kukaa" alisema Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA aliendelea kueleza kuwa "Matibabu ya awamu ya tatu ya Tundu Lissu yatafanyika nje ya nchi haitakuwa tena Kenya wala Tanzania, lakini kwa sababu za usalama hatuwezi kusema atakwenda sehemu gani au nchi gani, ukifika wakati sahihi tutasema hiyo awamu ya tatu ya matibabu itakuwa ya muda mrefu kidogo" alisema Mbowe
Mbali na hilo Mbowe ameendelea kusema kuwa serikali inafahamu watu ambao wameshambulia Tundu Lissu na kudai wao hawana imani na vyombo vya dola nchini na kusema vyombo hivyo vimekuwa tawi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo hawana nia ya dhati katika kufanya uchunguzi juu ya sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi mnamo Septemba 7, 2017.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hebu usijibaraguze, hata wewe 'mwenyekiti wa maisha' unawafahamu walompiga risasa tundu lisu, na kwa sababu gani.......kwani tukio hilo halina tofauti na lile la Chacha Wangwe .... a time will tell!!

    ReplyDelete
  2. Hivyo huyu kaka, Hana la maana zaidi katika maisha ya kila aiku...???
    ukiamka lisu... ukilala losu.
    saangapi utayashughulikia ya watu waliokuwa HAI.
    MANAKE TUSINGEKUJUA KAMA AI WATU WA HAI KUKUPA WEQE MWANA HAI KUINGIA BUNGENI NI WAHAI.
    NA UNAWAMINYIA WANA HAI KATIKA KUTAFUTA UHAI.
    HATA WEMA ULIKUWAGA UNAMPIGIAGA.
    ANGALIA YAKO KABLA HAYAJAKUSHINDA NA ULETE SERA ZA MAENDELEO.

    ReplyDelete
  3. Hivyo huyu kaka, Hana la maana zaidi katika maisha ya kila aiku...???
    ukiamka lisu... ukilala losu.
    saangapi utayashughulikia ya watu waliokuwa HAI.
    MANAKE TUSINGEKUJUA KAMA AI WATU WA HAI KUKUPA WEQE MWANA HAI KUINGIA BUNGENI NI WAHAI.
    NA UNAWAMINYIA WANA HAI KATIKA KUTAFUTA UHAI.
    HATA WEMA ULIKUWAGA UNAMPIGIAGA.
    ANGALIA YAKO KABLA HAYAJAKUSHINDA NA ULETE SERA ZA MAENDELEO.

    ReplyDelete

Top Post Ad