Baada ya Kifo Chenye Utata cha Mwanafunzi Mkoani Kilimanjaro Polisi Wamshikilia Mkuu wa Shule

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya Kifo Chenye Utata cha Mwanafunzi Kilimanjaro Polisi Wamshikilia Mkuu wa Shule
Kamanda wa Polisi kwenye Mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah anaethibitisha kwamba tarehe 10 November 2017 ndio Polisi walipata taarifa rasmi kuhusu kifo cha utatanishi cha Mtoto ambae ni Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Scolastica iliyopo Himo Moshi Kilimanjaro.

Kamanda Issah ameendelea kwa kusema “Tulifanya mahojiano tukianzia na Mmiliki wa Shule, Walinzi na Majirani na baadhi ya Wanafunzi,  katika mahojiano hayo kuna baadhi ya watu tuliwazuia ili kuendelea na uchunguzi”

“Tukishirikiana na Familia ya mtoto ambae alipotea ilikuja na plan B ambayo ilitusaidia na walisema mtoto wao tayari ameshafariki na moja kwa moja wanahusisha kifo hicho na Mmiliki wa hiyo shule” – Kamanda Issah

Makundi ambae ni Baba Mdogo wa Marehemu amesema “Tulipata taarifa ya mtoto kupotea tarehe 7 japo hatukua tunajua alipotea lini, tulivyopata taarifa tukatoka Dodoma kuja kufatilia na kwenda shuleni kwao na kiukweli taarifa tulizozipata shuleni zilikua haziridhishi kutokana na mazingira tuliyoyakuta”

“Wakati tunafatilia kwa kushirikiana na Shule na watu wengine na kituo cha Polisi cha Himo tukawa tumepata taarifa kwamba kuna Mwili uliokotwa mtoni karibia na shule ya Scolastica” – Makundi

Polisi Kilimanjaro bado inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na inamshikilia Mkuu wa shule hiyo ya Scolastica,
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad