BOT Yaeleza Kuwa Tanzania Miongoni mwa Nchi za Afrika Ambazo Uchumi Wake Unaokua kwa Kasi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

BOT Yaeleza Kuwa Tanzania Miongoni mwa Nchi za Afrika  Ambazo Uchumi Wake Unaokua kwa Kasi
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeeleza  kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika katika kipindi cha muongo mmoja uliopita yaani kuanzia mwaka 2007  hadi  2016.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchumi BoT, Johnson Nyella jana jumatatu kwenye sherehe ya Siku ya Takwimu Afrika (2017), iliyofanyika kitaifa jijini Dar es Salaam ambapo alieleza kuwa  uchumi wa Tanzania ulikua kwa wastani wa asilimia 6.7 mwaka 2016, wakati pato la taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7, sawa na ilivyokuwa mwaka 2015 na 2014.

Bw. Nyella amesema  kwa miaka minne mfululizo, mfumuko wa bei wa Taifa umeendelea kupungua na kubaki katika kiwango cha tarakimu moja.

“Mwaka 2016 mfumuko wa bei ulipungua na kufikia wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.6 mwaka 2015 na asilimia 6.1 mwaka 2014.” amesema Nyella huku akielezea umuhimu wa Takwimu bora.

Takwimu bora za uchumi zinahitajika katika kupanga mipango ya maendeleo na utungaji wa sera kwa ajili ya kuboreshamaendeleo endelevu ya mwaka 2030.

Kwa mujibu wa Nyella, takwimu bora za kiuchumi zinasaidia kuongeza tija serikalini katika kupanga mipango ya maendeleo na kukabiliana na changamoto kadri zinavyojitokeza.

Amesema takwimu bora pia zinawasaidia watunga sera na watekelezaji wa programu mbalimbali na kupanga mikakati mipya ya kuboresha maisha ya wananchi.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa amesema kwenye sherehe hizo kuwa, takwimu bora za uchumi ni muhimu katika kufikia ajenda ya Bara la Afrika ya mwaka 2063 inayosisitiza ukuaji wa uchumi.

Katika kufikia ajenda hiyo, baadhi ya mambo yanayosisitizwa ni amani, utulivu, kuboresha uchumi wa Afrika, kukusanya mapato ya Afrika ili Afrika iweze kujitegemea.

Dk Chuwa, amesema Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi ya Afrika (UNECA) kwa kushirikiana na Ofisi za Takwimu za Afrika, ina kaulimbiu isemayo “Takwimu Bora za Uchumi kwa Maisha Bora” ikisisitiza umuhimu wa takwimu za kiuchumi katika kuleta maendeleo endelevu hivyo kuboresha maisha ya wananchi.

Kaulimbiu hiyo inaakisi juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais John Magufuli kwa kuwa na dhamira ya kutengeneza uchumi wa viwanda. Amesema kwa sababu hiyo, takwimu rasmi za uchumi za serikali lazima zitolewe kwa weledi na kwa kufuata kanuni na sheria.

“Takwimu bora za uchumi kwa nchi yetu ni za muhimu sana, hasa wakati huu ambao Serikali yetu inaimarisha uchumi wa viwanda ili Tanzania iweze kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 na kuboresha zaidi maisha ya wananchi. Takwimu hizi za uchumi ni pamoja na takwimu za kilimo, viwanda, ujenzi, usafirishaji, nishati, biashara, mazingira, mfumuko wa bei na uwekezaji.”amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema takwimu bora ni takwimu zilizo sahihi, zinazotolewa kwa wakati, linganifu na za kina, zinazozalishwa mara kwa mara na zenye ufanisi. Dk Chuwa alisema, sifa hizo zote zinaendana na kanuni za msingi za takwimu rasmi za Umoja wa Mataifa na Mkataba wa Takwimu wa Afrika, ambazo maisha ya wananchi, hasa kutekeleza ajenda.

Chanzo:HabariLeo
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad