Dully Sykes Awatupia Lawama Wasanii wa Bongo Fleva

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dully Sykes Awatupia Lawama Wasanii wa Bongo Fleva
Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes amewalalamikia wasanii wadogo kiumri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kukosa upendo na umoja baina yao kwa kutokupeana sapoti kwenye kazi zao.

Dully amesema Wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye muziki ambao amewaita madogo hawana upendo wala umoja katika kusapotiana na kudai kuwa sio tu kwa wasanii wakongwe bali hata hao wenyewe kwa wenyewe na kuwafananisha na mdudu Kaa.

“Vijana wa sasa hivi wanatakiwa wajifunze kupendana, vijana wa sasa hivi hawapendani yaani hawana mapenzi, hawana ule upendo wamekuwa kama Kaa, Mimi nilijaribu kutuma posti yangu (ya wimbo mpya) juzi nikitegemea kupata nguvu nyingi kutoka kwa vijana lakini imekuwa tofauti na nilivyofikiria kwani wazee wenzangu ndio wamenipa sapoti akina Rich One, akina Mwana FA ndio walinisapoti na ndio walikuwa na furaha, kuna vijana wengine mpaka wanasema  kwamba nimetoa wimbo lakini hawajui  kama mimi nimetoa wimbo, wengine wanasema nitakupostia lakini hawaposti.“amesema Dully Sykes kwenye mahojiano yake na Radio Free Afrika Kwenye kipindi cha New Chapter na kuwapa ushauri wasanii hao

“Sasa mimi naomba tu kuwambia wale vijana ambao wanahisi labda muziki ni wa kwao peke yao hapana.. Unajua Mungu sisi wengine sisi ametupa utofauti mimi nakula majani kama Twiga wakae watulie, hao watakula majani chini kama Mbuzi, mimi nitakula ya juu, Wakae watambue kuwa wasishindane na Tembo wataumiza makalio.”

Soma na Hii – Hili ndio jibu la Dully Sykes kwanini wimbo wake mpya kauita ‘Bombardier’

Dully Sykes kwa sasa anafanya vizuri kwenye Media na wimbo wake wa Bombardier ambao umewavutia watu wengi kwenye aina ya uandishi hadi video ya wimbo huo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad