Mahakama Imemuhukumu Miaka 20 Jela kwa Kukutwa na Kucha 17 za Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama Imemuhukumu Miaka 20 Jela kwa Kukutwa na Kucha 17 za Simba
Meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater ambae leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam imemuhukumu kwenda jela kwa miaka 20 baada ya kupatikana na hatia.

Pater amehukumiwa kwenda jela miaka 20 au kulipa faini ya Shilingi Milioni 534 baada ya kukutwa na kosa la kupatikana na kucha 17 za Simba.

Hukumu hiyo imetolewa leo November 22, 2017 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, ambapo amesema amesikiliza ushahidi uliotolewa na Mashahidi wanne wa upande wa mashtaka, vielelezo vitatu na utetezi wa Mshtakiwa mwenyewe.



Hakimu Mkeha amesema Mahakama imemkuta na hatia Mshtakiwa huyo baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi hiyo pasipo kuacha shaka na kueleza kuwa vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani hapo ni kucha za Simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo mshtakiwa alishindwa kulipa faini na kupelekwa gerezani.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad