Mahakama: Wema Hakufanyiwa Upekuzi Kwenye Viungo Vyake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mahakama: Wema Hakufanyiwa Upekuzi Kwenye Viungo Vyake
November 1, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepokea kielelezo cha hati ya ukamataji mali nyumbani kwa Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa serikali, Elizabeth Mkunde kusema kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi.

Katika uamuzi wake, Hakimu Simba amesema amepitia hoja zote za upande wa mashtaka na utetezi kuhusu hoja za kupokelewa ama kutopokelewa kielelezo hicho, ambapo ameona akipokee.

“Mahakama inatupilia mbali pingamizi la utetezi la kutaka kielelezo kisipokelewe, hivyo nimekubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kielelezo kinapokelewa,”

Hakimu Simba amesema sababu za kupokea kielelezo hicho ni kwamba Wema hakufanyiwa upekuzi kwenye maungo ya mwili wake bali ni nyumba yake, hivyo haina tatizo kama ilipekuliwa na askari wakiume.

” Kama upekuzi ungeusu maungo ya mwili wake basi kungekuwa na tatizo, lakini umefanyika nyumbani kwake,”.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi November 16/2017.

Mbali ya Wema katika kesi hiyo, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa  na Matrida Abbas ambapo wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad