Rais Magufuli Amwagia Sifa Kikwete Kwa Kufanikisha Ujenzi wa Hospitali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Amwagia Sifa Kikwete Kwa Kufanikisha Ujenzi wa Hospitali
Rais wa Serikali ya awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa sifa na pongezi kwa rais mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kufanikisha ujenzi wa hospitali ya Mloganzila.

Rais ametoa pongezi hizo leo wakati akihotubia wananchi waliohudhuria ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam.
“Wakati ujenzi wa Hospitali hii unaanza mimi nilikuwa naagizwa tu na niliambiwa nikatafute eneo kubwa nikawaza nitalitoa wapi lakini baadae mzee Jakaya akanipigia tena simu  akaniambia kuna eneo huko Mloganzila ni la serikali nenda kaangalie na ujenzi uanze haraka, ndio nikaja hapa”, amesema Rais Magufuli.
Rais magufuli ameongeza kuwa “Watu tunapenda sifa lakini hizi sifa sio zangu ni za rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwani mimi nilikuwa naagizwa tu nikiwa waziri wa Ujenzi, ndio maana nimeona niseme wazi kuwa sifa zote zimwendee mzee Kikwete”.

Aidha rais Magufuli ameweka wazi kuwa wakati anakwenda kuona eneo la Mloganzila wala hakukuwa na barabara lakini aliambiwa na rais Kikwete aanze ujenzi wa miundombinu ikiwemo barabara haraka iwezekanvyo na alifanya hivyo sambamba na waziri wa maji amnbaye naye aliagizwa kuanza ujenzi wa miundombinu ya maji.
Rais Magufuli amesisitiza kuwa kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila jijini Dar es salaam ni mpango na jitihada za rais wa awamu ya nne.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si alikuteua bwana. Ni nfugu. Na tunalipana bwana. Pia bado tunalindana. Tulipeana kiapo cha kuto kusalitiana. Ni kufichiana yaliyopita na kupska mafuta mazuri watanzania wayanuse na kusahau yote yaliyopita ikiwa mikatsba na kuachia nchi kuliwa na kumilikishwa kwa wachsche na kiudugu. Ndo vita ya sasa kuziba midomo ya wale waliohamia ccm waliokuwa vitidhio kwao. Sasa ni marafiki. Wamepoa wakidhani mwidho wa vita. Hays. Tuone wapi Tanzania itaelekea na kwa maneno matamu gani.

    ReplyDelete

Top Post Ad