Serikali Yaiomba Mahakama Kumuongezea Kifungo Oscar Pistorius

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Yaiomba Mahakama Kumuongezea Kifungo Oscar Pistorius
Serikali ya Afrika Kusini imeiomba Mahakama ya juu nchini humo kumwongezea kifungo mwanaridha mlemavu, Oscar Pistorius ‘Blade Runner’ aliyekutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp, Februari 2013.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Pretoria, Thokozile Masipa, alimhukumu Pistorius kifungo cha miaka sita baada ya kumtia hatiani kwa mauaji ya bila kukusudia, uamuzi ambao  haujawaridhisha watu

Hivi karibuni, serikali hiyo kupitia Wakili, Andrea Johnson, ilirejea mahakamani na kuomba uamuzi wa Jaji Masipa ubatilishwe na mwanaridha huyo aliyejipatia umaarufu kwa kushiriki mbio akitumia miguu ya bandia kwa kuwa ni mlemavu, aongezewa muda zaidi wa kukaa jela.

“Jaji aliyeisikiliza kesi alikosa kabisa kuweka wazi sababu za kutotoa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka 15 (Kwa mujibu wa sheria za Afrika Kusini) alipomhukumu Oscar Pistorious kwa mauaji ya Reeva Steenkamp,” wakili huyo aliiambia mahakama hiyo ambayo bado inaisikiliza rufaa hiyo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad