Tanzia: Mbunge wa Songea Mjini Gama Kuzikwa Kijijini Kwao Likuyufusi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tanzia: Mbunge wa Songea Mjini Gama Kuzikwa Kijijini Kwao Likuyufusi
Aliyekua mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama anatarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.

Gama aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 24,2017 atazikwa Jumatatu Novemba 27,2017 katika makaburi hayo yaliyopo umbali wa kilomita 25 kutoka Songea mjini.

Akizungumza na Mwananchi Issa Fussi ambaye ni msemaji wa familia na mdogo wa Gama amesema amefariki usiku wa kuamkia leo akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho.

Amesema Gama alikuwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na alipelekwa hospitalini hapo Jumatano Novemba 22,2017 usiku na kulazwa hospitalini hapo .

Fussi amesema msiba huo ni pigo kwa familia kwa kuwa Gama alikuwa nguzo akitegemewa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kifamilia.

Amesema mwili wa marehemu Gama umehifadhiwa katika Hospitali ya Peramiho na utaratibu wa mazishi unaendelea.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad