Zitto Kabwe Aizungumzia Bombadier Bungeni....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali imekiri kujitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji wa shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), ambao serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga Septemba 21 mwaka 2011.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mh. George Mkuchika wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Kabwe lililohoji kwanini serikali imejitoa kwenye Mpango wa Kimataifa wa uendeshaji serikali kwa uwazi (OGP).

Mh. Mkuchika amesema baada ya serikali kushiriki kwenye utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, ambapo ameongeza kuwa sio nchi ya kwanza kujitoa kwenye mpango huo.

“Baada ya serikali kushiriki utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa miaka minne imeamua kujitoa, na Tanzania sio nchi pekee iliyojitoa, zipo nchi kama Hungury na Urusi zilijiunga na baadae kujitoa”, amesema Waziri Mkuchika.

Kwa upande mwingine Mh. Zitto ameshauri kuwa serikali ingeendelea kuwa mwanachama wa (OGP) ingefaidika kwa sulaa la ndege za Bombadier ambazo zimekwama nchini Canada kutoka na nchi huyo kuwa ndiyo mwenyekiti wa sasa wa OGP.

Hata hivyo Waziri amesisitiza kuwa mahusiano ya Tanzania na Canada ni mazuri bila hata ya Tanzania kuwa mwananchama wa (OGP) ambapo masuala ya Bombadier yatashughulikuwa na balozi wa Tanzania nchini humo.

Mpango wa kuendesha serikali kwa uwazi ulizinduliwa Septemba 20 mwaka 2011 na rais wa zamani wa Marekani Barack Obama ikiwa kama taasisi binafsi. Hadi sasa umoja huo una nchi wanachama 70 ambapo nchi 10 pekee ndio zinatoka barani Afrika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad