Zitto Kabwe, Hana Mpango wa Kurudi CHADEMA- Addo Shaibu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe, Hana Mpango wa Kurudi CHADEMA- Addo Shaibu
Msemaji wa chama cha ACT Wazalendo, Addo Shaibu, amesema kiongozi wa chama hicho ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Zuberi Kabwe, hana mpango kabisa wa kurudi CHADEMA, licha ya kuwa na harakati kama zao na kuomba ushirikiano wao.

Addo Shaibu ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba licha sasa hivi ACT Wazalendo kimeamua kuendeshwa kiharakati kama ilivyo CHADEMA, na licha ya kutaka kuunganisha nguvu katika baadhi ya mambo ambayo yataupa ushindi upinzani, lakini ifahamike kuwa hana mpango wa kurudi huko.
“Tunajua kwa nini Zitto aliondoka, alikuwa na mgogoro na CHADEMA, na ndio sababu ya kuanzisha ACT, wakitazama lugha yake kwamba wapinzane tushirikiane wanaona kama lugha yake na CHADEMA imekuwa haina tofauti, mazingira ya kisiasa ndio yanalazimika hivyo, mambo wanayoyapitia CHADEMA na sisi tunayapitia, inalazimisha lugha iwe ya pamoja, hatuwezi kuunganisha vyama, na nakuhakikishia Zitto hana mpango kwa sasa wa kurudi ndani ya CHADEMA”, amesema Addo Shaibu.
Hivi karibuni Zitto Kabwe alisikika akiomba ushirikiano kutoka kwa vyama vya upinzani hususan CHADEMA ili kuweza ksuhinda kwenye chaguzi ndogo ndogo za udiwani zinazokuja, na kuibua hisia kuwa huenda chama hicho sasa kinataka kujiunga na CHADEMA kuwa pamoja.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Zitto zuberi Kabwe hakuondoka kwetu.
    TULIMFUKuZA MSALITI HUYU.
    ASIJIBABAISHE..
    HATUMTAKI KAMWE.
    LOWASA KAJA NA FEDILIKI PIA TUNAE.
    ZITTO KAMA CHAMA CHAKE KINATAKA KUFUNGWA KWA AJILI YA KUKOSA QUORUM INAYOHITAJIKA KISHERIA KUNA NA HAKI YA KUWA CHAMA.
    BASI WACHA KIFE PEKE YAKE.
    HATA WANACHAMA MAHIRI WANAMKIMBIA KABLA .
    ZITTO KUWA MJASIRI AMALI UUZE ILE BIASHARA.

    ReplyDelete

Top Post Ad