Zitto Kabwe. Jambo moja Linanisumbua sana...Nisaidieni Tafadhali

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Anaandika Mbunge wa Kigoma Zitto Kabwe.
Jambo moja linanisumbua sana. Nisaidieni tafadhali

Inawezekanaje Serikali ikasaini mkataba wa shilingi Trilioni 7 kujenga Reli bila kuweka vifungu vya kufungamanisha na sekta nyengine nchini? Yani kweli hata misumari ( screws) nchi hii haiwezi kutengeneza mpaka iagizwe kutoka Uturuki? Yani hata kampuni ya kuchimba kokoto itoke Uturuki? Hivi Viwanda vya Chuma nchini vinafanya kazi gani sasa? CTI, TPSF nielezeni hili, hamuwezi kuzalisha kitu chochote kulisha ujenzi wa Reli ya Kati ya SGR? Katika BOQ ya Mradi wa SGR, hamna muwezalo? Serikali iliwapa BOQ mkashindwa? Ukiwauliza watu wa Wizara hawana majibu, wanasema Mkataba ali negotiate Rais mwenyewe. Inawezekana kweli? Siwezi kumwuliza Rais. Anasema sisi kazi yetu kukosoa tu. Amekasirika. Siwezi kumwuliza mtu aliyekasirika, tena Amiri Jeshi Mkuu.

Wakati wa Mdororo wa Uchumi Asia mwaka 1997-1998 Waziri Mkuu wa Malaysia Tun Mahathir Mohammed alifanya miradi mikubwa sana ikiwemo kujenga Mji Mpya, barabara kubwa na Jengo la Petronas. Kwanini? Ili kuingiza fedha kwenye uchumi na kuchochea shughuli nyengine za uchumi na kukuza mahitaji ( aggregate demand). Malaysia ikawa nchi ya kwanza kuibuka kutoka Asian Financial Crisis.

Sisi Watawala wetu wamekwenda madarasa tofauti na kusoma vitabu tofauti vya Uchumi? Unajenga Reli kwa pesa yako ( inavyodaiwa), kwa hiyo unakusanya kodi kutoka kwa watu wako, unanunua US$, unamlipa Mkandarasi. Mkandarasi ananunua kila kitu kutoka nchini kwao Uturuki, mataruma ya Reli, Chuma, Screws na Misumari na hata mchimba kokoto Mturuki. Kwenye uchumi hii inaitwa leakages. Uchumi wetu unahitaji more inflows.

Unajengaje Reli kwa kutumia Chuma kutoka nje the wakati una hazina ya chuma Ludewa? Unamwaga TZS 7 Trilioni bila kuhakikisha offsetting? Natamani kuiona hiyo BOQ ya Reli ya Kati.
Hili linanisumbua sana. Siamini kuwa watawala waliokwenda shule na wenye uzoefu Serikalini hawakuona faida kubwa ya offsets. Baraza la Mawaziri limejaa PHDs, kweli wameshindwa kuona hili? Fedha zetu wenyewe tunatengeneza ajira nje? Kwamba sisi tuwe vibarua tu na wagonga reli? Trilioni 7 zingechochea sana uchumi ( multipliers).

Tunaambiwa sisi tupo negative mno. Hebu watetezi wa Serikali, mnaojua kuitafsiri Serikali, nisaidieni. Hili mnaona lipo sawa?
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndo maana utawala wa ccm unakataa kusaini katiba mpya ya Warioba. Wote wahusika wanaozidi kulipeleka taifa hili na kulipotosha inabidi wachukuliwe hatua kali wasaini au wasisain katiba mamilioni ya watanzania wasikubaki mtu mmoja adictate nchi iwe maskini. Awe na uwezo wa kufikiri wa kujua afanyalo au asiwe nao, kuna mawaziri, washauri nao wawajibishwe kwani wamekabidhiwa kuisaidia serikali ili itende vipasavyo.ni hawa mawaziri mizigo yes sir no sir ili tu wasifukuzwe na mkuu wao na kutetea vyeo na mishahara minono ambayo ni kodi za watanzania maskini wanaomwamini kuwa anawstetea kumbe anawachukulia hata kile kidogo walichonacho kukipeleka nje. Inabidi hii mikataba idimamishwr mara moja.ni ujinga kabisa. Nyerere alisema adui mkubwa wa maendeleo nchini ni ujinga. Mtu mjinga hafundishiki hata.kukubali kuendeshwa kijinga ni kukubali kulipeleka taifa tena kwenye umaskini na tusikubali.

    ReplyDelete
  2. Ni aibu kwa Taifa zima. Kuto kujielewa unachokifanya na kutokupokea ushauri wowote hii nchi bado wageni ndio wapatao faida. Ooo inauma. Na kamabibauma itumike njia kumwelimisha mtu asiyejijua ni nini afanyalo. Labda hajui.

    ReplyDelete

Top Post Ad