Makazi ya Muda ya Mama Samia Yakaguliwa na Waziri Mkuu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makazi ya Muda ya Mama Samia Yakaguliwa na Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua matengenezo ya makazi ya muda yanayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan atakapohamia Dodoma.

Waziri mkuu amefanya ukaguzi huo leo Jumatano, Desemba 6, 2017 mchana  katika eneo la Kilimani mjini Dodoma ambako yalikuwa makazi ya mkuu wa mkoa.

Akitoa taarifa ya ujenzi, Waziri wa Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Wenye Ulemavu na Vijana, Jenista Mhagama amesema kikosi kazi cha kuratibu kazi ya Serikali kuhamia Dodoma kilibaini mahali alipokuwa akiishi awali si sahihi kwa ajili ya makazi ya kudumu ya Makamu wa Rais.

“Pale palikuwa panafaa kwa ajili ya ziara za kikazi alipokuwa akija Dodoma, kwa hiyo tumeamua tufanye ukarabati hapa ili aweze kuishi kwa viwango vinavyostahili,” amesema katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Amesema kazi ya matengenezo itagharimu Sh1.5 bilioni wakati kazi ya kutenganisha ofisi za watumishi na wasaidizi wa Makamu wa Rais itagharimu Sh680 milioni.

Waziri mkuu pia amekagua matengenezo ya ofisi inayotarajiwa kutumiwa na Makamu wa Rais ambayo itakuwa eneo la Ndejengwa.

Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma, Steven Simba anayesimamia ujenzi huo amesema wanataraji kazi itakamilika kabla ya Desemba 30,2017.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu zangu. Msitumie pesa nyingi hivi..

    ReplyDelete

Top Post Ad