Mambosasa Akanusha Kutupilia Mbali Kesi ya Dkt Shika "Kesi Ipo Pale Pale Tukitaka Kumpeleka Mahakamani Umma Utajulishwa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mambosasa Akanusha Kutupilia Mbali Kesi ya Dkt Shika "Kesi Ipo Pale Pale Tukitaka Kumpeleka Mahakamani Umma Utajulishwa"
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amekanusha taarifa za kuachana na kesi ya Dkt.Louis Shika, na kusema kwamba kesi yake bado ipo pale pale isipokuwa hawajaipa kipaumbele.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Kamanda Mambosasa amesema jalada la kesi ya Dkt. Shika bado lipo isipokuwa kesi yake haina mashiko kwani hajaleta madhara yoyote kwenye nyumba zilizokuwa zikipigwa mnada.
Kamanda Mambosasa amesema iwapo wataamua kumpandisha mahakamani Dkt. Sika kujibu mashitaka yake umma utajulishwa ili wajue kile kinachoendelea.
"Siyo kweli kama tumeamua kuachana naye kabisa, jalada lake lipo na likikamilika tutaamua nini kinafuata, Shika hakuleta madhara yoyote hivyo kesi yake haina public interest, nyumba ziko salama na hajadhuru mtu, tukiamua kumpandisha mahakamani tutaujulisha umma ili wajue", amesema Kamanda Mambosasa.
Dkt. Louis Shika amefunguliwa jalada la kesi kwa kosa la kuharibu mnada wa nyumba za Lugumi ambao upo kwa amri ya serikali, kwa kusema ananunua nyumba hizo kwa milioni 900 ilhali mfukoni hana pesa kabisa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hii ni Bora kwa Usalama wake ...Jalada likae wazi na aendelee Kuripoti.

    ReplyDelete

Top Post Ad