Mamia Wafurika Dodoma Kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mamia Wafurika Dodoma Kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 56 ya Uhuru
Wakazi wa mji wa Dodoma na viunga vyake mapema leo Jumamosi, Desemba 9, 2017 wamejitokeza kushuhudia maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Taratibu za ukaguzi wa kiusalama, zilifanya misururu mirefu baada ya kutumika geti moja kuingilia ndani ya Uwanja wa Jamuhuri.

Hali hiyo ilifanya misururu mrefu kuanzia geti la kuingilia uwanjani kufika katika barabara inayoelekea Nkuhungu.

Mabasi makubwa yanayotoka katika wilaya za jirani yalionekana yakishusha watu tangu saa 11.00 alfajiri kuwahi foleni.

Watu walianza kuingia uwanjani huku vikundi mbalimbali vya burudani vikitumbuiza.

Saa 2:00 asubuhi, gwaride maalumu lililojumuisha vikosi vya ulinzi na usalama viliingia uwanjani.

Viongozi mbalimbali walianza kuwasili uwanjani kuanzia saa 1:00 asubuhi wakiwemo mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mama Fatma Karume, mke wa Rais ya Kwanza wa Tanzania Mama Maria Nyerere na aliyekuwa makamu wa kwanza wa Rais, Mohammed Gharib Bilal.

Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema ni baadhi ya viongozi wa kisiasa walioonekana uwanjani hapo.

Viongozi wengine waliofika asubuhi uwanjani hapo ni Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, mke wa Rais, Janeth Magufuli, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin Mkapa, majaji wakuu wa makatibu wakuu wa wizara mbalimbali, Spika wa Bunge Job Ndugai, mawaziri na wabunge.

Tayari Uwanja wa Jamhuri umejaa na wananchi wamezuiwa kuingia katika uwanja huo na milango yote imefungwa.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Milimonyi Wawaha....!!!

    To Muze Kwi Dodoma.... Na Mkulu yazaaa Kukaya... Mlungu yamtaze.
    Wadodo Waswano kukaya...
    Karibuni Dodoma ... Jisikieni mko nyumbani kama tulivyo waambia. Milango yetu na Nyoyo Zetu Ziko Wazi.
    Mama Samia... Mkulu Mwaha JPJM.... Karibuni Sana.... Majali Mtoto wa Nyumbani.
    Na ugeni wako wote mnakaribishwa ..karibuni sana Tunafuraha kuona mko nyumbani.
    Tunamuomba Mungu akuzidishieni Upendo Na kila Mara muwe mnakuja.
    Dodoma yetu ina Historia yake na Wamepita watu wengi wakubwa na Mpaka sasa Tunajivunia kwa uamuzi wa Marehemu Baba wa Taifa alipoamua kuipa Daraja la Makao Makuu.
    Lakini alichofanya Baba Magu na Uamuzi wa Kijasiri na Kufuatilia Utekelezaji wa Mh. K Majali
    Nasema kwa furaha kubwa kuwa Umefanya Kazi katika awamu hii yetu ya Tano na Hakika Hapa Kazi Tu.

    Uhuru ni Majukumu na Wabebaji haya Majukumu ni Mimi Na Wewe kat
    ika Kuileta Tanzania yetu Mpya.
    Tanzania Oyeee.... Wazalendo Oyeeeee... JPJM na Watendaji wake Mahiri Oyeeeeeeee.
    Mungu Akubarikini Sana.... Na Karibuni Sana Dodoma.

    ReplyDelete

Top Post Ad