Mjadara Mkali Waibuka Baada ya Mbunge wa Chadema Kujiudhulu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Barua na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikieleza mbunge wa Siha (Chadema) mkoani Kilimanjaro, Dk Godwin Mollel amejiuzulu ubunge imezua mjadala.

Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema akizungumza na MCL Digital leo Alhamisi Desemba 14,2017 amesema naye ameona video na barua kwenye mitandao ya kijamii lakini hawana uthibitisho wowote.

"Mheshimiwa Mollel hakuwahi kuonyesha dalili yoyote kuwa yuko kwenye hilo wimbi na mimi nimeona hiyo barua na video kwenye mitandao. Bado kwangu nachukulia kama uvumi mpaka tutakapothibitisha," amesema.

Lema amesema kwa utaratibu alipaswa kumuandikia barua Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe au viongozi wa Chadema.

Amesema akiwa katibu wa mkoa wa chama hicho hajapokea barua yoyote kutoka kwa Dk Mollel.

"Ukiangalia hata barua inayosambaa haijasainiwa na video inaonyesha ni mtu tu kajirekodi akarusha. Katika mazingira hayo hatuwezi kukurupuka kuzungumzia hilo jambo," amesema.

Taarifa inayosambaa kwenye mitandao ambayo haina saini inaonyesha kuandikwa na Dk Mollel akieleza ameamua kujivua uanachama wa Chadema kuanzia leo Alhamisi Desemba 14,2017.

Pia, ametangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge na kwamba huo ni uamuzi wake alioufanya akiwa na akili timamu na hajashinikizwa na mtu yeyote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dkt Mollel ni kweli amejiuzulu baada ya kutafakari na kufatilia kwa muda Mrefu Uongozi wa Serikali hii ya awamu ya Tano Chini ya DkT Magufuli.
    Baada ya kukaa naye aliweza kunena baada ya kujiuliza na kupata Majibu yake yote na Kuhisi Ushirikiano wake unahitajika katika Jimbo letu la Siha Utapatikana kwa njia ya CCM na hii ni CCM Mpya.
    Umahiri wa Mwenyekiti wa Sasa wa CCM hauna kifani na Dkt Mollel ameamua kumpa USHIRIKIANO STAHIKI KWA MANUFAA MAPANA YA NCHI YETU>
    CCM OYEEEEE< DKT MOLLEL OYEEEEEEEE> MAGUFULI OYEEEEEEEEE. CCM MBELE KWA MBELEEEEEEE

    ReplyDelete
  2. tehetehetehe ama-kweli-mwaka-wa-hasara-ni-hasara-tu, hata-ukipanda-mchicha-inaota-bangi-mara-paaap-askari-hawa-hapa-jela-ina-kuhusu!! Piiiippooozzz PWAAAAAAAA!!

    ReplyDelete

Top Post Ad