Mtoto wa Gadafi Ajitokeza Kugombea Urais wa Libya 2018

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtoto wa Gadafi Ajitokeza Kugombea Urais wa Libya 2018
Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Libya Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, anatarajia kugombea urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao mwaka 2018.


Taarifa za Saif al-Islam kutaka kugombea nafasi hiyo ambayo baba yake alikuwa ameishikilia kwa muda wa miaka 42, ilitolewa na msemaji wa familia Basem Hashimi Soul.

"Saif al-Islam atagombea urais kwenye uchaguzi ujao ambao unaweza ukafanyika katikati mmwa mwaka 2018,ana dhamira ya kuongeza ulinzi zaidi na utulivu kulingana na jografia ya Libya, kwa kushirikiana na makundi yote ya Libya, hivi karibuni anatarajia kuweka wazi tarahe ya kujitangaza rasmi kwenye vyombo vya habari", amesema msemaji Basem Hashimi Soul.

Nchi ya Libya hivi karibuni imekuwa isiyo ya utulivu, kutokana na vurugu zinazoendelea, huku mtoto huyo wa Gaddafi akiwa na imani kubwa Umoja wa Mataifa utakubaliana nae katika kipindi hiki kigumu ambacho nchi hiyo kinaipitia, cha kutafuta utulivu.

Saif al-Islam ni mtoto wa pili wa Muammar Gaddafi ambaye alitolewa madarakani na kuuawa mwaka 2011, na pia ni mwanasiasa mwenye utaalam wa uchumi.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad