Nani Yupo Sahihi, Afande Sele au Mrisho Mpoto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Maneno Makali ya AFANDE SELE kutoka Instagram Kwa MRISHO MPOTO na Majibu ya MPOTO kwa AFANDE SELE...

Afande Sele King - Rafiki yangu mkubwa mjomba mpoto kama ni kweli wewe ndio ulikua kinara ktk kusimamia utayarishaji wa wimbo maalumu wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa halafu ukashawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa ndani ya wimbo huo na badala yake ukampa nafasi rafiki yetu christian bella kushiriki ktk wimbo huo unaowahusu watanzania wkt ukijua wazi kuwa bella pamoja na ukweli ni rafiki yetu sana lkn bado yeye sio mtz bali ni mcongoman....ktk hili mjomba umetukosea sana watanzania wenzako na kwa hakika kama ingekua kitendo chako hicho umekifanya kwa nchi zilizoshiba uzalendo na zisizovaa joho la unafki mjomba ulistahili kukatwa nywele zako na kupigwa risasi angalau tano kichwani kwa uchache tena hadharani kwani ulichofanya ni usaliti kwa nchi yako na ni aina flani ya uhaini...

Majibu

Mrisho Mpoto Akijibu - Kaka yangu @afandeseleking Bado narudia kusema kwamba heshima nnayokupa inatoka Mbali sana kwenye chumba cha nne cha moyo Wangu... Sihitaji kupoteza wino Mwingi kukukumbusha tofauti iliyopo kati ya UZALENDO, UZAWA na URAIA kwasababu nina uhakika unazifahamu vyema isipokuwa huenda leo haujaamkia ule ubavu sahihi na ule wa ukarimu wako ulionao siku zote, mpaka ukakataa uwepo wangu hapa Duniani Kwa kunichagulia adhabu ya kupigwa risasi tano tena za kichwa... kwakua hukuniuliza hili jambo kabla Itoshe kusema hunitaki tena...hivyo basi kabla sijapigwa hizo risasi tano nitakachofanya ni kukupa maelezo machache yatakayokufanya uipate picha ya UZALENDO.. Hivi unajua kama John Okello alipigania uhuru wa Zanzibar!? Majeshi yetu yamepigania uhuru wa msumbiji na hata Chegu sio mcuba na alipigania uhuru wa Cuba na Congo pia.. Na je unajua kama kuna wazawa wanaoangamiza maslahi ya nchi na kuna wazalendo wasiobagua!? Kaka, Afrika ni moja na waafrika wote ni ndugu zetu ( umajumui Afrika, tena ukichimba huko sana kwa hapa nchini utakuna na Prof Shivji) .. na ndio maana hata mwenge wa uhuru uliwekwa juu ya mlima kilimanjaro ili kumulikia nchi nyingine.. Kumbuka hiyo mitizamo ya KIUZAWA Mwalimu aliita mitizamo membamba.. kwa maana ya kwamba ipo kwa ajili ya Kuiangamiza afrika

Na mwisho ningependa kukuuliza--->Je umezisikia shangwe za wazalendo na wazawa leo hapa dodoma baada ya kusikia Babu Seya na familia yake wamepewa msamaha wa rais!!? Wewe ni RASTA kaka.. kumbuka siku zote CHUKI HUMUUMIZA ANAYEIHIFADHI.. #AfrikaUnite ✊


Nani yupo sahihi kati ya hawa mafahari wawili? 
Je kuwa Mzalendo ni lazima uwe mzawa wa nchi husika?
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad