Ngoma Awasili Nchini Awaangukia Viongozi Yanga

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ngoma Awasili Nchini Awaangukia Viongozi Yanga
SIKU chache baada ya kutokea taarifa za mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma aliyekuwa kwenye matibabu nchini Zimbabwe kuteuliwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo, nyota huyo amewasili nchini na kujitetea kwa viongozi.

Ngoma amewasili nchini juzi na kwenda kuonana na viongozi wa timu hiyo ambao walionekana kushangazwa na kukasilishwa na kitendo cha Ngoma kudanganya kuumwa huku akiitwa kwenye kikosi cha timu yake ya taifa.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh, akizungumza na gazeti hili jana, alisema Ngoma amerejea nchini na kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na uongozi kuweka mambo sawa.

“Ngoma amerejea na mimi mwenyewe nimeongea naye, ameandika barua kwa katibu kuelezea safari yake kwenda Zimbabwe kwenye matibabu,” alisema Saleh.

Aidha, alisema kuwa mshambuliaji huyo alikataa kuwa ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo kilichokuwa kishiriki michuano ya Chalenji.

“Amesema hajaitwa kwenye timu ya taifa ila alionana na kocha wa timu hiyo na alimueleza kuwa yupo (Zimbabwe) kwa ajili ya matibabu,” alisema.

Suala hilo sasa lipo kwa viongozi na wanaendelea na mazungumzo.

Kwenye mtandao wa Chama cha Soka cha Zimbabwe iliandikwa kocha wa timu ya Taifa ya nchi hiyo, Sunday Chidzambga, amemjumuisha Ngoma kwenye kikosi chake kwa ajili ya michuano ya Chalenji.

Hata hivyo kwa sasa kuna taarifa Zimbabwe imejitoa kwenye michuano hiyo ya Chalenji inayoanza kesho kwa kile walichoeleza kuwa usalama Kenya ni mdogo.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad