Lema Amsindikiza Nassari Polisi Kutoa Taarifa ya Tukio la Uvamizi Nyumbani Kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lema Amsindikiza Nassari Polisi Kutoa Taarifa ya Tukio la Uvamizi Nyumbani Kwake
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akiwa na Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wameenda kwenye kituo cha polisi Usa River kutoa taarifa ya tukio la uvamizi uliofanyika nyumbani Nassari usiku wa kuamkia leo Jumamosi.

Tukio hilo limetokea Kijiji cha Nkwanekori wilayani  Arumeru mkoa wa Arusha.

Katika ukurasa wake wa Twitter Nassari ameandika, “Nimevamiwa nyumbani kwangu maeneo ya USA RIVER usiku huu na watu wenye silaha, na kufyatua risasi ambazo zimeua mbwa waliokuwepo nje ya nyumba. Nimefanikiwa kukimbia na mke wangu na kuripoti kituo cha Polisi. Nimekuwa nikitishiwa kuuawa kila siku, sina amani ndani ya nchi yangu.”

Baadhi ya majirani na viongozi wa Chadema wamefika nyumbani kwake kumjulia hali na baadaye kumsindikiza kituo cha polisi Usa River.

Mmoja wa majirani ambaye hakupenda kutajwa jina lake amesema alisikia milio ya risasi zaidi ya 12 na baadaye kimya kutawala.
Chanzo Mwananchi
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Lema Unajifanya Msamaria......Ma, Mtanfanyiaje mwenzenu halafu mnampeleka kwenye Usalama.
    Huu Mchezo Hauridhishi.... Na kama mlisha fanya kule siku zile kwa sasa mnakwenda na msigwa kumwangariaga.
    Huu mchezo hauna Tija... Kama mnataka kumwibia na Ujambazi wenu. Kwa Nini MUUE MBWA kani Si Viumbe pia?
    Sasa Idadi ya Lisasi ngapi mpaka mkapoteza Maisha ya Viumbe Viwili ya Nassiri.
    Je Nassiri alimpeleka akiwa na Hali gani kutoa Ripoti na Mao Viumbe lazima wafanyiwe uchunguzi kabla ya Kuzikwa hapo Vetenari hospitali kujua idadi na aina ya Risasi.
    Pole Nasiri kwa kupotelewa na hao Wawili.
    Jitahidi uongeze idadi na hao wanajifanya kuja hapo wala usiwajulishe manake wahenga alinena
    KIKULACHO SIKU ZOTE.............Mwako.... Ndio Hao hao.

    ReplyDelete
  2. Pole Jusua.....Pole kwa kupotezewa maisha ya hawa wawili.
    usiogope kivuli chako dogo, ukilikorogaga utalinywaga pasi na shaka
    Sasa WEWE unatafuta kadi bila kumwaga mwenyekiti hapo.
    huko unapotaka kwenda umewataarifu na wemekukubali kuwa watakuchukua?
    Jiangalie Dogo.... Watakufanyizia hawa Hawana Mwamana...

    ReplyDelete
  3. Joshua Si Umesikia hata Wema pia Amerudi....

    Pole Jusua.....Pole kwa kupotezewa maisha ya hawa wawili.
    usiogope kivuli chako dogo, ukilikorogaga utalinywaga pasi na shaka
    Sasa WEWE unatafuta kadi bila kumwaga mwenyekiti hapo.
    huko unapotaka kwenda umewataarifu na wemekukubali kuwa watakuchukua?
    Jiangalie Dogo.... Watakufanyizia hawa Hawana Mwamana...

    ReplyDelete
  4. Mimi sio mtaalamu wa makosa ya jinai lakini hili tukio la kuvamiwa kwa huyu Nassari hakika lina kila dalili yakuwa ni mchezo wa kuigiza au movie alieitengeneza yeye mwenyewe na muhusika mkuu au staring ni yeye mwenyewe. Nassari watu watake kumua kwa tishio gani alinalo kisiasa? Labda majamabazi kutaka kumpora lakini niliangalia maelezo yake binafsi ya Nassari akilalama kana kwamba vyombo vya dola ndivyo vilivyo husika na tukio hilo. Jamani? Vyombo vya dola au serikali ikitaka kumfanyia uhalifu raia haiwezi kumkosa kwani wana watu ambao ni well trained sio rahisi mtu kama Nassari akajibizane risasi na usalama wa taifa au askari polisi alafu Nassari atoke salama hivyo ni vitu vya kuchekesha sana. Kuna sababu nyingi ya Chadema na Nassari kutengeneza hii movie inayoitwa watu wasijulikana. Sababu ya kwanza (1) siasa za matukio...baada ya Chadema na upinzani kukosa hoja za msingi za kushindana na CCM matukio yakuunda na ya kutengeneza ndio imekuwa mtaji wa kutafutia mvuto wa kisiasa kwa wanachama wao na wananchi. Sababu ya pili. Hakuna asiejua yakwamba chama cha Chadema kinakwenda zake kuzimu hilo halina shaka lakini wahusika wanataka kuaminsha ulimwengu yakwamba kufa kwa Chadema ni kutokana na uonevu wa serikali ya chama cha mapinduzi kitu ambacho sio kweli. Sera mbovu za Chadema. Muundo m'bovu wa chama ukanda na umimi ndio halibadri inayoiua Chadema. Sababu ya tatu ni..Siasa za hofu. Hofu ni mmoja ya kati ya mtaji wa maana katika harakati za kumiliki hisia za watu. Wakati mwengine hofu hutumika hata kutawala watu iwe katika mapenzi, ndoa, kazini nakadhalika hofu ni silaha muhimu . Chadema na upizani wanatumia hofu kama mtaji wa kisiasa ili kuvuruga mawazo ya watanzania ili waondowe imani juu ya serikali yao inayowaongoza. Sababu ya nne ya Chadema na upinzani kutengeneza siasa za matukio ni kujaribu kuzishawishi jumuiya za kimataifa baada ya kugonga ukuta hapo mwanzo yakwamba utawala uliokuwepo hivi sasa Tanzania si utawala wa sheria na haki ni wa udikteta, ni njia moja ya Chadema kujitafutia sapota na misaada kutoka mataifa ya nje hata kama ni kuichafua nchi yetu katika jumuiya za kimataifa. Ikumbukwe wazungu Mjerumani,Muengereza na wengineo walizitawala nchi za kiafrica na kuiba kila kitu mpaka watu kwa mamia ya miaka sio miaka mitano 5 au kumi 10 na hakuna waliposhitakiwa some time you can see how stupid as Africans we are in believing white people. Na kwa hili tukio la Nassari kila mtu anajua yakwamba kama uchaguzi utafanyika leo wa ubunge pale katika jimbo lake basi Nassari hawezi kushinda tena hata CCM wakimsimamisha mgombea mpumbavu . Hata matokeo ya chaguzi za madiwani, upinzani hawakuibiwa wala nini wamepigwa haswa kihalali kabisa na hata kama ukirejewa tena hii leo si ajabu Wapizani wakapoteza hata hicho kiti kimoja wichopata. Watanzania wamechoshwa kudanganywa na wapinzani. Wamechoshwa na ahadi hewa za wapinzani na wamebaini ili mabo yao yaende lazima wailete serikali karibu na wanapoishi. Na hawawezi kuileta serikali karibu na wanapoishi kama hayaja wachagua wagombea wa chama tawala. Na kwa bahati nzuri Magufuli anajitahidi kuhakikisha watendaji wake wanakuwa watendaji wa watu hasa wanyonge na kuhakikisha wanawajali. Katika falsa ya utendaji uliotukuka katika kuwahudumia wananchi,watendaji wa serikali siku zote huwa watumwa na wananchi ndio mabosi na serikali ya Magufuli inakaribia utukufu huo kwa hivyo upinzani bado unasafari ndefu kuin'goa CCM na katika kuchanganyikiwa huko kwa upinzani ndiko kunakowapelekea kuzua mambo wengi ya ajabu ili kusavaivu kisiasa.

    ReplyDelete
  5. Swadakta Mdau ,Hapo Juu nakubaliana nawe kwa asili mia kwa mia.
    Hawa sisi tuna waelewa na wao wanajijua.
    Mbinu zao na Hulka zao na upotoshaji wao vyote vinajulikana.
    Na hivi sasa wenye akili na mwelekeo wote wameamua kuondoka.
    Huyu mwendesha chama kisaccos amepoteza Dira na Mwelekeo.
    Kitambi ana mengi ya kutujuza vimilieni kidogo mtakuja kuelewa Bayana.

    Vitimbi vyenu vinaeleweka na Havitusumbui wala IGP Sirro kumshughulisha vileee.

    ReplyDelete

Top Post Ad