AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Mkurugenzi wa Idara ya habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akizungumza na waandishiwa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelelezo uliopo jengo la LAPF mjini Dodoma
Dkt. Abbasi ameyasema hayo mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya maoni ya wataalam wa uchumi kutoka IMF ambao wamemaliza ziara yao hapa nchini Desemba 12, 2017.
“Ripoti ya IMF inaonesha katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017 uchumi umekua kwa asilimia 6.8, takwimu ambazo ni za juu katika chumi zinazokua kwa kasi na ikizidi nchi kadhaa zilizofanyiwa tathmini mwaka 2017 zikiwemo za Ulaya,” amesema Dkt. Abbas.
Aidha, kutokana na usambazaji mzuri wa chakula mfumuko wa bei ya chakula ulishuka hadi kufikia asilimia 4.4 ikiwa ni chini ya lengo ambalo IMF ilitabiri mfumuko ungekuwa asilimia 5.
Aidha amesema, Serikali imeendelea kulipa madeni ya ndani ambapo mpaka sasa Shilingi bilioni 900 zimeshalipwa na shilingi bilioni 37 zimelipa madeni ya watumishi wa Serikali.
Timu hiyo ya wataalamu kutoka IMF iliongozwa na Bw. Mauricio Villafuerte ambapo walifanya ziara juu ya tathimini ya uchumi katika nchi Saba Afrika ikiwemo Tanzania pamoja na Msumbiji, Rwanda, Nigeria, Uganda, Senegari na Cape Verde.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK