Takukuru Yawakalia Kooni Makada CCM Kuhusu Tuhuma za Rushwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Takukuru Yawakalia Kooni Makada CCM Kuhusu Tuhuma za Rushwa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Mwanza, imeendelea kuwang’ang’ania viongozi na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuendeleza uchunguzi dhidi yao kuhusu tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa uchaguzi uliomalizika Desemba 3,2017.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Mwanza, Ernest Makale leo Alhamisi Desemba 7,2017 ameieleza MCL Digital kuwa taasisi hiyo inaendelea kukusanya ushahidi ili kuwafikisha mahakamani au kuwaachia viongozi na makada hao ambao hata hivyo hakuwa tayari kuwataja.
Ninachoweza kukuthibitishia ni kwamba, tunaendelea na uchunguzi; ukikamilika tutawajulisha na hatua zingine za kisheria zitafuata,” amesema Makale.
Desemba 2,2017 maofisa wa Takukuru wilayani Ukerewe walilikamata na kulipekua gari la Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo alipokuwa katika kampeni za kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika Desemba 3,2017 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Akiwahutubia wana CCM baada ya kutangazwa mshindi kwa kura 555 dhidi ya kura 520 za mshindani wake wa karibu Saidi Mecky Sadiki, Diallo alielezea kitendo cha gari lake kupekuliwa hakikuwa cha kiungwana kwa sababu yeye ni muumini wa vita dhidi ya rushwa ambayo ni adui wa haki kupitia imani na ahadi yake ya mwana CCM.
Siku ya uchaguzi, maofisa wa Takukuru waliwakamata viongozi wanne wa CCM kutoka wilayani Ukerewe kwa tuhuma za kukutwa wakigawana Sh400,000 zikiaminika kuwa za rushwa kutoka kwa mmoja wa wagombea.
Makale alisema waliokamatwa, kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana wakati uchunguzi ukiendelea ni Gabriel Gregory, diwani wa kata ya Bukindo na mwenzake, Nicholaus Munyoro wa kata ya Murutunguru; Steven Mzige, Mwenyekiti wa CCM kata ya Muriti na Katibu wa Uenezi wilayani Ukerewe, Musa Manka.


----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad