Van Gaal Aibuka na Kuishambulia United kwa Mpira Mbovu Pamoja na Mkurugenzi wao

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jose Mourinho alitua Manchester United kuchukua mikoba ya kocha Mdachi Louis Van Gaal jambo ambalo hadi leo Mdachi huyo amekuwa akililalamikia sana kwa jinsi alivyoondolewa United.

Van Gaal amekuwa mkimya sana na hazungumzii sana maisha yake yalivyokuwa United lakini safari hii LvG ameibuka na kuishambulia Manchester United akidai kwamba wanacheza kpira mbovu.

Baada ya mchezo kati ya Manchester City zidi ya Manchester United Van Gaal amesema United hawavutii kuwatizama kwa sasa na kama utamuuliza anapenda kuingalia timu gani ni Man City.

Van Gaal amesema wakati yupo Manchester United alikuwa akicheza zaidi mchezo wa kushambulia lakini wapinzani walikuwa wakizuia tofauti na sasa ambapo United wanaonekana kuzuia zaidi.

Kuhusu kuwa na bifu kati yake na Mourinho ,LVG amesisitiza kwamba hana ugomvi na Mourinho ila ana tatizo na mkurugenzi wa klabu hiyo Ed Woodward kutokana na namna ambayo mkurugenzi huyo alimfukuza kazi Van Gaal.

Kinachomuuma zaidi Van Gaal ni namna ambavyo mke wake alifahamu kufukuzwa kwake ambapo LVG anadai mkewa aligundua kuwa Van Gaal anafukuzwa wakiwa kwenye lift na familia ya Woodward.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad