"Afrika Yaazimia Kuzalisha Umeme"- Majaliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

"Afrika Yaazimia Kuzalisha Umeme"- Majaliwa
Waziri Mkuu Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Waziri Majaliwa ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza baada ya mkutano wa viongozi wa wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli na kusema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

"Nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia mapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa ina mikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali", alisema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita ambapo ni pamoja na tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

"Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC", alisisitiza Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo  kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad