AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
John Feely ,rubani wa ndege wa jeshi la wanamaji alisema kuwa ilikuwa heshima kubwa kwake kujiuzulu.
Idara ya maswala ya kigeni ambayo inasimamia mabalozi wa Marekani iligundua kwamba amejiuzulu baadaye mwezi Disemba.
Kujiuzulu kwake hakukusababishwa na matamshi ya Trump ya hivi majuzi akiyataja mataifa ya Afrika na lile la Haiti kuwa ''shimo la kinyesi''.
''Kama afisa mdogo anayehusika na maswala ya kigeni, nilikula kiapo kumuhudumia rais na utawala wake hata iwapo sitakubaliana na sera kadhaa'', bwana Feely alisema katika barua yake ya kujiuzulu.
''Washauri wangu walianimbia kwamba iwapo naona siwezi kuhudumu tena basi ilikuwa heshima kujiuzulu.Wakati huo umefika''.
Katibu wa kudumu wa wizara ya maswala ya kigeni Steve Goldstein alithibitisha kwamba anajua kwamba bwana feely alitaka kuondoka kabla ya matamshi ya rais Trump ya siku ya Alhamisi.
Alisema kwamba balozi huyo ambaye alikuwa akifanyia kazi Marekani ya Latini alikuwa akiondoka kutokana na sababu zake za kibinafsi.
Baadhi ya sera za rais Trump zimesababisha hisia kali , ikiwemo hatua yake ya hivi karibuni kufutilia mbali vibali vya kuishi kwa raia wengi wa El Salvado, Haiti na Nicaragua wanaoishi nchini Marekani baada ya majanga.
Bwana Feely sio afisa wa kwanza wa wizara ya maswala ya kigeni kujiuzulu.
Elizabeth Shackeford aliehudumu mjini Nairobi kwa ujumbe wa Marekani nchini Somalia alijiuzulu mwezi Disemba.
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK