Hii Hapa Kauli ya Sumaye kwa Wanaohama Chama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hii Hapa Kauli ya Sumaye kwa Wanaohama Chama
Waziri Mkuu mstaafu na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ukanda wa Pwani, Fredrick Sumaye amedai wabunge na madiwani wanaohama vyama na kupelekea uchaguzi kufanyika tena ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi na ufisadi pia.

Mwanasiasa huyo akizungumza na kituo cha runinga cha Azam amesema mtu kuhama chama kimoja kwenda kingine haina shida lakini mtu anapohama labda kwa kushawishiwa au kwa sababu za maslai binafsi si sawa.

“Kama haya yanayotokea ni kwa sababu ya matumizi ya madaraka ama matumizi ya fedha hili jambo tulikemee sote,” amesema.

“Huwezi kutoka mbunge ama diwani kutoka Chadema/CUF ukaingia CCM halafu wakakuteua uende kwenye eneo lile lile, hii ni kuchezea fedha za wananchi kwa sababu ni kodi za wananchi, huo ni usifadi mkubwa,” amesisitiza.

Kwa kipindi cha mwaka jana wabunge watatu walijiuzulu na kuhamia vyama vingine, waliojiuzulu ni Lazaro Nyalandu, Maulid Mtulia,  Dkt. Godwin Mollel, pia kumekuwa na idadi kubwa ya madiwani wanaohama vyama.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alaaa kumbeee, mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
    Hahahaha alipohama Nyalandu mlichekelea na wala hamkuona ni kuchezea fedha wala ufisadi.......CDM wame-bip CCM wame-wapigia.... ngoma droooo! Piipoozzz PWAAA!!

    ReplyDelete

Top Post Ad