"Dawa ya Muhuni ni kuwa Muhuni zaidi" -Mwenyeti wa Chadema BAVICHA Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, BAVICHA, Patrick Ole- Sosopi amekiri kuwa Chama chake kimeamua kurudi kwenye uchaguzi mdogo haswa wa Kinondoni na Siha kwa kuwa wagundua dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi.


Akizungumza kwenye Kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa Kinondoni Salum Mwalimu Ole-Sosopi amesema kwamba kilichowafanya kususia uchaguzi mara ya kwanza ni kwamba hakukuwa na faida kubwa ya kupatikana kiongozi kwa wananchi wasio na hatia kwa kumwaga damu.

Ole-Sosopi amesema kwamba baada ya kususia uchaguzi ambao uligomewa kupelekwa mbele sasa wagundua kuwa "dawa ya muhuni ni kuwa muhuni zaidi hivyo ifahamike na iwekwe rekodi kuwa CHADEMA tumerudi na kushiriki na kufanya uchaguzi".

Mbali na hayo Ole-Sosopi ameongeza kuwa hataki chama chake au kingine kisipendelewe bali waachwe wabishane kwa hoja na mwishowe wananchi waachiwe kufanya maamuzi.

CHADEMA walitangaza kugomea uchaguzi mdogo uliofanyika January 13 kwa madai mbalimbali ikiwepo kufanyia hujuma za wazi katika uchaguzi uliofanyika Novemba 26 huku tume ikilalamikiwa kutofanyia kazi malalamiko hayo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sosopi... Ukizidi Uhuni siku hizi... Ile Kitu itapiga shoti halafu Virusi inaingia.. Kwisha Habari.!!!
    Halafu sisi tunazika..!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad