Jux Ajitolea Kumsomesha Mtoto Mmoja wa Shilole

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jux Ajitolea Kumsomesha Mtoto Mmoja wa Shilole
Msanii wa viwango kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, Juma Jux amejitolea kumsaidia msanii 'Shilole Baby' majukumu ya kumsomesha  mtoto wake mmoja kwa mwaka mzima ikiwa kama zawadi yake ya siku ya sherehe ya harusi iliyofanyika jana Jijini Dar es salaam.


Akizungumza jana katika sherehe Shilole na mume wake Uchebe, Jux amesema kwamba anafahamu kuwa mwanamke huyo ni mpiganaji na huwa hachoki kupambana katika kutafuta riziki yake mwenyewe na si tegemezi kwa mtu.

Akizidi kutoa sifa kwa Shilole kabla ya zawadi Jux amesema kwamba licha ya kuwa Shilole ni msanii mwenzake lakini pia wao ni marafiki ambao wanashauriana na kutaniana mambo mengi lakini pia anatambua kuwa ana mzigo wa majukumu ya kifamilia.

"Shilole ni mpambanaji sana sana. Ni mwanamke ambaye anaamini kwenye kutafuta kipato chake mwenyewe na siyo kupewa. Kwa kulitambua hilo nataka nimpunguzie mzigo kidogo dada yangu, Nitagharamia ada ya mtoto wake mmoja pamoja na mahitaji mengine kwa mwaka mmoja. Naamini nikifanya hivyo nitakuwa nimemsaidia yeye kuweza kusonga mbele katika mapambano mengine" amesema Jux.

Jana maeneo ya Masaki Shilole alifanya Sherehe ya harusi yake ambayo ilihudhuriwa na mastaa kibao wa filamu na muziki. Shilole alifunga ndoa ya kimya kimya  na mumewe Ashraf 'Uchebe' Mwanzoni mwa mwezi Disemba na jana ndiyo siku waliyoamua kufanya sherehe.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad