“Kama Odinga Ataapishwa Itadhihirisha Kuwa Afrika ni Tundu la Choo”- Mutua

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

“Kama Odinga Ataapishwa Itadhihirisha Kuwa Afrika ni Tundu la Choo”- Mutua
Wakati wananchi wa Kenya wakisubiria kwa hamu tukio la kuapishwa kwa Kiongozi wa Umoja wa Vyama vya Upinzani nchini humo (NASA) Raila Odinga, Gavana wa Kaunti ya Machakos Dkt. Alfred Mutua amesema kuwa kama tukio hilo litafanikiwa kufanyika basi ni dhahiri kuwa bara la Afrika ni tundu la choo.


Dkt. Mutua amesema kuwa Kenya itakuwa nchi ya kwanza duniani kuapisha marais wawili katika awamu moja.

“Kama hili la kuapishwa kwa kiongozi wa NASA litafanikiwa basi utakuwa mfano mzuri utakaodhihirisha kuwa bara letu ni mfano wa Tundu la Choo. Mtu utawezaje kuapishwa wakati huo huo kuna kiongozi mwingine ameshaapishwa na Jaji Mkuu? hii ni aibu kwa bara letu,“ameandika Dkt. Mutua kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Neno ‘Tundu la Choo’ limewa maarufu zaidi duniani baada ya Rais Donald Trump wiki mbili zilizopita kutamka nchi za Afrika na Haiti ni mfano wa ‘Tundu la Choo’.

Kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya anatarajiwa kuapishwa Januari 30, 2018 na kuwa Rais wa watu wengi kama anavyojiita.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wamarekani huwa na wanatafsiri tofauti kabisa na tafsiri ya kiengereza cha kawaida na ndio maana waliofahamu vizuri maneno aliyotamka raisi wao walilaani sana. Kwa sababu ni matusi mazito na si maneno ya kuyarejea mara kwa mara kuyatamka. Matamshi ya tundu la choo linalojadiliwa na kupigiwa kelele na kulaaniwa na wengi ni tundu la choo lilopo baina ya makalio ya mtu, waswahili wa neno lao maalum ya sehemu hiyo. Sasa Africa kufanananishwa na sehemu ya kutolea kinyesi sidhani kama ni sawa ingawa kuna wengine wanaona poa tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad