Kisa Lissu Bavicha Yamvaa Shaka Hamdu wa UVCCM Yasema ni Kichaa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Bavicha Yamvaa Shaka Hamdu wa UVCCM Yasema ni Kichaa
Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Julius Mwita amefunguka na kusema kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka huenda ana matatizo ya akili.


Mwita amesema hayo leo Januari 11, 2018 katika Mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu tuhuma alizotoa kiongozi huyo wa UVCCM dhidi ya Tundu Lissu ambapo alisema kuwa Tundu Lissu ni muongo na hapaswi kuaminiwa kwani atafuta tu umaarufu.

Kufuatia kauli hiyo ya Shaka ndipo hapo viongozi wa Baraza la Vijana wa CHADEMA walipoaamua kujitokeza na kuzungumzia juu ya kauli hizo za kijana wa CCM na kusema kuwa "Tumetafakari kauli ya Shaka kwa kina na tumejaribu kufikiri kama Shaka ana akili timamu au ni kichaa? Kwa sababu kama chama chake chenyewe wamekiri pamoja na Serikali hawawezi kuzungumza suala la Lissu kwa sababu ni mgonjwa na yupo hospitali, Shaka anapata wapi ujasiri wa kuja kuzungumza mambo yanayomuhusu Tundu Lissu tena kwa kuzungumza mambo ya uongo na ushahidi usio na tija yoyote na anawadanganya Watanzania kuwa katika nchi hii Lissu siyo wa kwanza kupigwa risasi" alisema Mwita

Aidha kiongozi huyo wa BAVICHA amemtaka Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka alisimame na kusema mpaka sasa Tundu Lissu ametibiwa kwa fedha ya Serikali shilingi ngapi.

"Tulitegemea umoja wa vijana wa chama ambacho kinaendesha Serikali watoke wawaambie Watanzania kwamba tunakitaka chama chetu yaani kiiagize Serikali kutibu mgonjwa ambaye yupo hospitali na ameshambuliwa katika majukumu yake ya Ubunge lakini Shaka anatoka kupotosha kwa maneno ya kejeli na ya kihuni. Lakini tumkumbushe Shaka, Amani Abed Karume hakuuawa kwa sababu za kisiasa na wala hajawahi kuwa mpinzani, wala hajawahi kuwa mkosoaji wa Serikali iliyopo madarakani kwa wakati huo useme kwamba alishambuliwa kwa sababu ya ukosoaji wake bali kulikuwa na sababu zingine tofauti zilizopelekea Karume kushambuliwa"

Siku kadhaa zilizopita Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu alifunguka na kuishtumu Serikali ya awamu ya tano kuhusika katika kushambuliwa kwake baada ya kali hiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Shaka Hamdu Shaka naye amlijibu Tundu Lissu na kusema kuwa mwanasiasa huyo ni muongo na anatafuta umaarufu.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na wewe unaesema Abeid Amani Karume hajauwawa kwa sababu ya siasa si tu unamatatizo ya akili bali ni Mpumbavu vile vile. Waliotuhumiwa kumuua Karume kule Zanzibar pengine wengine mpaka hivi tunazozungumza wangali hai na kama wameshapita mbele ya haki vizazi vyao vingali hai kawaulize nini maana mtu kutuhumiwa au kuhukumiwa kwa kosa la uhaini?

    ReplyDelete

Top Post Ad