Mbowe Asikitishwa na Kauli ya Lowassa Kuisifia Serikali Asema " Siwezi Kujibishana na Lowassa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mbowe Asikitishwa na Kauli ya Lowassa Kuisifia Srikali Asema " Siwezi Kujinishana na Lowassa"
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amefunguka na kutoa msimamo wa chama chake kuhusu kitendo alichofanya Mjumbe wa Kamati Kuu ya (CHADEMA), Edward Lowassa kwenda Ikulu na kumsifia Rais Magufuli kwa utendaji wake.


Mbowe amesema kuwa kauli mbalimbali alizotoa Lowassa jana si msimamo wa chama chake na kudai kuwa amesikitishwa na kauli za kiongozi huyo kuisifia Serikali ambayo wao wanaona hajatenda hata hayo ambayo amejaribu kuyasifia.

"Siyasemi haya kubishana na kauli alizozitoa Mhe. Lowassa, pengine yeye anazo takwimu zake tofauti ambazo tunazijua kwa sababu amezungumzia kuhusu ajira lakini hakusema kutolewa kwa ajira ngapi? Japo imelinganishwa na ujenzi wa reli ya kati unaweza ukaongeza ajira, Naona kuna tatizo kubwa la ajira katika nchi, na kuna ongezeko kubwa la vijana wengi ambao hawana ajira, tunatambua wanamaliza Shule hawapati ajira, lakini vile vile kuna makampuni yanafungwa, biashara zinafungwa, benki zinaelekea kufungwa nafasi nyingi za ajira zinapotea" alisema Mbowe

Aidha Mbowe aliendelea kusisitiza na kuonesha masikitiko yake kwa kauli ya Lowassa jana  "Nisikitike tu kwamba sisi tuna kilio kikubwa, utakumbuka kwamba tunaendelea kumtibu Mhe. Tundu Lissu ambae alishambuliwa kwa risasi, unashindwa kupata ujasiri wowote, kiongozi wa CHADEMA kweli unamsifia Magufuli, wakati tunauguza watu, msaidizi wangu Ben Sanane amepotea, viongozi wetu wameuawa, wengine wamefungwa, Wabunge wanafukuzwa Bungeni, wakina Ester Bulaya, Halima Mdee kwa mashtaka ambayo ni ya kubambikiza ambayo hayafuati kanuni za Bunge" alisisitiza Mbowe

Mbali na hilo Freeman Mbowe ametoa kauli ambayo huenda ina ashiria kiongozi huyo kutaka kurudi kwenye chama chake cha awali CCM na kuachana na CHADEMA

"Kuhama watu kutoka chama kimoja kwenda chama kingine, haijawa jambo geni kwenye siasa za Tanzania, kazi ya kujenga Upinzani katika Taifa letu sio tukio la siku moja ni mchakato wa muda mrefu, lazima ipitie vipindi mbalimbali ambapo linafanya mchujo wa asili na kubakiza watu wachache ambao watasonga mbele wataleta uhuru wa kweli Maendeleo ya kweli na haki zote za kidemokrasia katika Taifa" alisema Mbowe

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe Mbowe ni mwenyekiti wa Chadema Taifa acha kulialia hovyo kwenye mitandao kama kinda la ndege. Edward Lowasa sio mtu mdogo kiumri hata kisiasa kwa hivyo kama unahisi kakukosea au kakikosea chama tafuta njia stahiki za kumfahamisha sio unaanza kumzalilisha kwenye mitandao ya kijamii. Kama sio Lowasa wakati huu wa mzee bulldozer Chadema ingekuwa tayari ipo kaburini. Hakuna baya alilosema muheshimiwa Lowasa nashangaa Mbowe anasikitiahwa na nini? Muheshimiwa Edward Lowasa anawafundisha siasa Mbowe na Chadema yakuwa siasa sio uadui. Na kama Mbowe umekereka zaidi mtimuwe Edward Lowasa kutoka Chadema kama unaubavu.

    ReplyDelete
  2. hahahahaha! 'Mugabe' chama kinakudodea, Lowasa hawezi unafiki, msema ukweli ni mpenzi wa Mungu piiiipooooozzzzzzz PWAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Top Post Ad