Mchezaji Bocco Anawajibu Waliobeza Kusajiliwa Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshambuliaji wa Simba John Bocco leo Januari 28, 2018 amefunga magoli mawili dhidi ya Majimaji na kufikisha magoli saba (7) kwenye msimu huu wa ligi ambapo raundi ya kwanza imemalizika baada ya kila timu kucheza mechi 15.

Bocco hakuanza vyema msimu huu, lakini alipata majeraha mapema kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Simba vs Mtibwa Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, ni mchezo huo ambao pia alishuhudiwa Salim Mbonde akishindwa kuendelea na mchezo baada ya kupata majeraha ya goti.

Kwa sasa Bocco amekuwa yule aliyetarajiwa na watu wengi, endapo anakuwa fiti kwa asilimia 100 shughuli yake mabeki wanaifahamu, asipofunga atatoa assist.

Katika mechi za hivi karibuni Bocco amefunga magoli muhimu ambayo yaliamua baadhi ya mechi, (Tanzania Prisons 0-1 Simba, Ndanda 0-2 Simba, Simba 4-0 Majimaji) Bocco amefunga mabao matano katika mechi hizo ambazo Simba ilifunga magoli saba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Azam ameungana na Obrey Chirwa (Yanga) Mohamed Rashidi (Tanzania Prisons) na Habib Kiombo (Mbao FC) wote wakiwa wamefunga magoli saba.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad