Ole Sendeka Amvaa Mange Kimambi Sakata la Kuvuja kwa Audio Inayosemekana ni Yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ole Sendeka Amvaa Mange Kimambi Sakata la Kuvuja kwa Audio Inayosemekana ni Yake
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka amefunguka na kumvaa mwanaharakati Mange Kimambi na kusema kuwa dada huyo anamchafua na kutaka kumgombanisha na viongozi wa nchi kwa kusambaza sauti ambayo si yake.


Ole Sendeka amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa hadhara wa CCM katika kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge wa jimbo la Longido Arusha kwa chama hicho na kusema hiyo sauti ambayo inasambazwa na huyo dada kuonesha kuwa anamzungumzia Rais John Pombe Magufuli vibaya pamoja na Bunge si sauti yake bali imetengenezwa na watu wa upinzani kwa lengo la kumchafua na kumchonganisha.

"Akutukanaye hakuchagulii tusi, kupitia mitandao ya kijamii wameendelea kutengeneza na kusambaza 'clip' za kutafuta namna ya kunifarakanisha mimi na viongozi wa Serikali nataka niwaambieni ambazo mmeziona kwenye mitandao zinasambazwa na watu wa upinzani pamoja na sijui Mange Kimambi sijui kitu gani kile, ninaomba mzipuuze kwa kiwango kinachostahili maana zote ni uzushi mtupu" alisisitiza Ole Sendeka.

Katika moja ya sauti ambayo ilikuwa inasambaa ikidaiwa kuwa ni ya Mkuu wa Mkoa huyo wa Njombe ilikuwa inasema kuwa Bunge sasa limeshikwa na kushindwa kufanya kazi yake jambo ambalo limempeleka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kujadili na kuchunguza kauli ya Mhe. Christopher Ole Sendeka inayodaiwa kudhalilisha Bunge.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad