Ray Afunguka Kuhusu Kumvisha Hereni Mwanaye "Mtoto wa Nyoka Ni Nyoka"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ray Afunguka Kuhusu Kumvisha Hereni Mwanaye "Mtoto wa Nyoka Ni Nyoka"
Msanii wa filamu, Vincent Kigosi maarufu ‘Ray’ amesema kitendo cha kumvisha mtoto wake hereni ni kutokana na kuwa nyota kama yeye.

Ray amesema hayo alipozungumza na MCL Digital baada ya kuweka hadharani picha za mtoto huyo wa kiume aliyevishwa hereni hivyo kuzua gumzo.

Maoni kadhaa yamekuwa yakitolewa kuhusu kitendo hicho pamoja na kunyolewa nywele staili ya kiduku.

Akizungumzia uamuzi wa kufanya hivyo kwa mtoto wake wa pekee aitwaye Jaden, msanii huyu aliyewahi kutamba na filamu za Oprah, Waves of Sorrow na Pretty amesema yeye ni nyota maarufu hivyo mtoto wake lazima afuate nyayo zake.

“Mbona mimi baba yake nimetoboa masikio watu hawasemi, si kwa kuwa wanajua mimi ni mtu maarufu, hivyo umaarufu huu nilionao hata mtoto lazima awe nao japo sijamtoboa sikio atakuja kufanya hivyo mwenyewe kama ataamua atakapokuwa mkubwa,” amesema.

Ray amesema, “Hao wanaosema waendelee tu kusema kwa kuwa kusema ni haki yao, na huyu ni mwanangu hakuna mtu wa kunipangia nini cha kumfanyia.”
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad