Wasichana Wang,aa Ufaulu Kidato cha Pili, Darasa la Saba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wasichana Wang,aa Ufaulu Kidato cha Pili, Darasa la Saba
Katibu Mtendaji Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA),Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa kwa wanafunzi wa kidato cha pili na darasa la nne huku wasichana wakiongoza (waking’ara).


Akizungumzia matokeo ya kidato cha pili,Dk Msonde alisema wanafunzi 433,453 ambao ni asilimia 89.32 wamepata ujuzi na maarifa ya kuwawezesha kuendelea na Kidato cha Tatu. Kati ya hayo wasichana ni 224,736 ambao ni asilimia 88.55 na wavulana ni 208,717 ambao ni asilimia 90.17.

Kwa upande wa kidato cha pili, wasichana wameshika nafasi zote 10 bora kutoka kwenye shule tatu za Feza Girls, Canossa na Precious Blood. Kwa darasa la nne, wasichana wameshika nafasi nane za juu na wavulana wakishika nafasi ya tisa na 10. Katika matokeo ya mwaka 2016, wasichana walikuwa wanane na wawili wavulana, na mwaka 2015 wavulana walikuwa watano na wasichana watano.

Aidha, Msonde alisema wanafunzi 51.807 ambao ni asilimia 10.68 wamefeli kwa kushindwa kupata alama za kuwawezesha kuendelea na kidato cha tatu. Mwaka 2016 wanafunzi 372,228 (asilimia 9.02) waliendelea na kidato cha tatu huku wanafunzi huku asilimia 8.98 ambao ni wanafunzi 36,737 walifeli.

“Somo ambalo wanafunzi wamefaulu zaidi ni Kiswahili kwa asilimia 91.92 na lile la ufaulu wa chini ni Hisabati yenye asilimia 32,” alisema. Akizitaja shule 10 zilizofanya vizuri kuwa ni Kemebos (Kagera), Canossa (Dar), St. Francis Girls (Mbeya), Marian Boys (Pwani), Kilimanjaro Islamic na Precious Blood (Arusha), St Augustine-Tagaste (Dar), Don Bosco Seminary (Iringa), Marian Girls (Pwani na Anwarite Girls (Kilimanjaro).
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad