Yanga Kuwakosa Kuukosa Mchezo wa Kesho Dhidi ya Azam FC

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Kuwakosa  Kuukosa Mchezo wa Kesho Dhidi ya Azam FC
Wachezaji saba wa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wataukosa mchezo wa kesho unaotarajiwa kuchezwa dhidi ya Azam FC katika dimba la Azam Complex kutokana na sababu mbalimbali walizokuwa nazo.


Hayo yamebainishwa leo na Afisa Habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kuwataja wachezaji kuwa ni Yohana Mkomola, Thaban Kamusoko, Amisi Tambwe, Abdallah Shaibu, Donald Ngoma pamoja na Patongonyani ambao wote hawa ni majeruhi huku Pius Buswita akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano alizozipata katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Azam FC ni wachezaji saba pekee ndio watakaokosa mchezo huo kama nilivyosema lakini kila kitu kimekamilika. Tunaiheshimu sana Azam kwani wamekuwa na msimu mzuri wanapata matokeo ndani na nje ya uwanja wao wa nyumbani ila ata sisi Yanga SC tupo vizuri na tunatarajia kupata matokeo kwenye mchezo wa kesho", alisema Dismas Ten.

Azam FC kesho itakuwa inamkaribisha Yanga SC katika dimba lao la nyumbani ambapo mchezo huo utachezwa majira ya 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad