Asasi za Kiraia Zapaza Sauti Zimetaka Tume Huru ya Uchanguzi Kuundwa Kuchunguza Mauaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Asasi za Kiraia Zapaza Sauti  Zimetaka Tume Huru ya Uchanguzi Kuundwa Kuchunguza Mauaji
Asasi za Kiraia nchini zimetaka iundwe Tume huru ya uchunguzi wa kifo cha Mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwiline itakayoundwa na Taasisi za Dini, Vyombo vya Habari, Majaji, Mahakimu, Polisi na Baraza la Vyama vya Siasa.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Equality for Growth, Jane Magigita amesema kuwa Asasi za kiraia zimesikitishwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Tunapendekeza iundwe Tume huru ya uchunguzi itakayohusisha Azaki, Taasisi za dini, vyombo vya Habari, Baraza la vyama vya siasa, wanahabari, Majaji, Polisi, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi juu ya vifo na vitendo vya utekwaji na utesaji,”-Magigita

“Pia ni kosa kubwa kuwaachia Polisi kujichunguza wenyewe katika matukio yanayowahusu,” -Magigita

Mbali na hilo, pia ameiomba Serikali itazame upya suala la upatikanaji wa Katiba mpya na mchakato wake uanze mwaka huu kwani ndiyo suluhisho la matatizo mbalimbali yanayotokea katika Jamii kwa sasa.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad