Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Champongeza Rais Magufuli

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) Champongeza Rais Magufuli
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi amepongeza Rais  John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.

 Ngwilimi ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama.

Pia, ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili, tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale inapostahili."

Ametoa wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji , makarani  na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo wanatakiwa  kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea, kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.

Pia  kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa yaliyotokea hapo nyuma

Ngwilimi ametoa  wito akisema: " Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo maabara , kama jumba la kamari.



----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yalaa weee!! Makamu mbona umeliamsha Tundu, ngoja tusubiri kusikia tamko lake kutoka kitandani...duh! TLS kumpongeza JPM...HAIWEZEKANI, tena ni makosa makubwa hahahaha......yaani sipati picha, kama namuona Lissu presha-inapanda-presha-inashuka....watu oyoooooooooooooooooooooooooooooooooooooHAPA-KAZI-TU!

    ReplyDelete

Top Post Ad