Hatimaye Familia ya Akwilina Anayedaiwa Kuuwawa na Polisi Imekabidhi Serikali Bajeti ya Maziko..... Ni Zaidi ya Milioni 80

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Familia ya Akwilina Imekabidhi Serikali Bajeti ya Maziko..... Ni Zaidi ya Milioni 80
Familia ya mwanafunzi wa kwanza katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), anayedaiwa kuuawa na polisi wiki iliyopita, Aquilina Akwilini imekabidhi serikali bajeti ya maziko ya zaidi ya Sh milioni 80.
Msemaji wa Familia, Festo Kavishe amekabidhi bajeti hiyo leo Jumanne Februari 20, kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwipalo na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisali Makori leo. "Hayo ndiyo makubaliano ya familia, tumewakabidhi wataenda na kujadiliana kisha tutakutana nao saa 10 jioni leo, kisha watatueleza ya kwao pia, tunachohitaji ndugu yetu apumzike kwa amani," amesema Kavishe.

Marehemu Aquilina ambaye aliuawa kwa risasi Ijumaa iliyopita akiwa katika basi baada ya polisi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliokuwa wakiandamana kwenda kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Wilaya ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao, anatarajiwa kuagwa Alhamisi wiki hii katika viwanja vya NIT na kusafirishwa Rombo mkoani Kilimanjaro, Ijumaa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tunalikubali hilo na tutamlipa. Na zaidi pia Fidia kwa Familia yake.
    Pia wasababishaji wa Hiki Kifo wakiongozwa na Fleman mtowe na genge lake la mtafaruku.
    tutawafikisha Kizimbani kujibu shataka la usababishaji wa kifo hiki na Fidia Husika juu ya mtoto huyu asiekuwa na hatia baada ya wao kuanzisha mtafaruku.
    Sisi kama ni Serikali Tumelikubali hilo na Ziada.
    Mungu amlaze mahali pema panapostahiki. Na tutaendelea kuwasiliana na Familia na Chuo na Genge la wahusika.

    ReplyDelete

Top Post Ad