Jalada la Walioisababishia Serikali Hasara ya Bilioni 2 Lafikishwa kwa DPP

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jalada la Walioisababishia Serikali Hasara ya Bilioni 2 Lafikishwa kwa DPP
February 13, 2018 Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya uhujumu uchumi wa kuisababishia hasara serikali ya bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini, Archard Kalugendo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya uchunguzi.

Mbali ya Kalugendo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu.

Wakili wa serikali,  Estezia Willson amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamikika.

Pia ameeleza kuwa jalada halisi la Kesi hivyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kwa ajili ya uchunguzi. Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi February 27,2018.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kuisababisha serikali hasara ya zaidi ya bilioni 2.4.

Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31, 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini walioajiriwa na Wizara ya Nishati na Madini waliisababisha serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad