Kifo cha Kingunge Chawagusa Wengi Wasanii Wamlilia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kifo cha Kingunge Chawagusa Wengi Wasanii Wamlilia
Wasanii wameungana kuomboleza kifo cha mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale -Mwiru aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo Februari 2,2018 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa takriban mwezi mmoja alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kung’atwa na mbwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Mwezi uliopita mkewe, Peras Ngombale-Mwiru alifariki dunia na Kingunge alitolewa kwa muda hospitalini ili kuhudhuria mazishi.

Kutokana na msiba huo, baadhi ya wasanii waliogushwa kwa kutumia kurasa zao katika mtandao wa Instagram wanaomboleza.

Msanii Chege Chigunda ameweka picha ya mwanasiasa huyo na kuandika, “lala salama.”

Jackline Wolper ameandika, “Nitoe pole kwa wafiwa wote na kwa familia ya mzee wetu Kingunge. Najua jinsi gani inauma kumpoteza baba, babu, mlezi na kiongozi pia.”

“Lakini Mungu kampenda zaidi na maumivu yanazidi hasa mama naye tumempoteza siku si nyingi hata arobaini bado na leo hii mzee wetu pia ametuacha. Mungu ana mitihani yake lakini kazi zake pia hazina makosa.”

“Poleni sana Watanzania wote! Mungu alaze roho ya mzee wetu mahala pema peponi...bwana ametoa, bwana ametwaa jina lake lihimidiwe,” ameandika Wolper.

Wasanii wengine walioomboleza ni Lady Jay Dee na Profesa Jay walioandika maneno, “Pumzika kwa Amani.”

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad