Lema Awasha Moto Bungeni Spika Kulipiwa Matibabu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Lema Awasha Moto Bungeni Spika Kulipiwa Matibabu
Mbunge  Godbless Lema amefunguka na kutoa malalamiko yake bungeni kuhusu kitendo cha Bunge kugharamia matibabu ya Spika wa Bunge Job Ndugai nchini India huku Mbunge Tundu Lissu mpaka sasa kutogharamiwa matibabu na bunge.

Lema amewasha moto huo wakati wakijadili taarifa ya Utawala bora, Katiba na Sheria na kusema kitendo ambacho Bunge linakifanya si haki na si sawa kwani ni undumilakuwili kuwapa watu wengine haki huku wengine wakinyimwa haki hiyo ya msingi.

"Kwanza nianze kwa kutoa pole kwa Spika Job Ndugai nafahamu yupo India kwa ajili ya 'checkup' na matibabu na vilevile Mhe. Lissu ambaye na yeye yupo Ubelgiji kwa ajili ya matibabu. Mhe Spika anatumia fedha za bunge na Serikali kwa ajili ya matibabu na ni mbunge wa bunge la Jamhuri ya Tanzania na Mhe. Lissu tumeendelea kumkusanyia pesa mitaani kwa vikopo na yeye vilevile ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hii 'double standard' inayoendelea katika taifa hili kwamba Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) anaweza kutibiwa na Serikali na Bunge na Mbunge anayetokana na upinzani aliyepigwa risasi Dodoma hawezi kutibiwa na bunge wa Serikali Mhe. Mwenyekiti Bob Marley ana wimbo unasema 'only time will tel'"
"Chief yupo oposition kapigwa risasi, kifungu namba 24 section one ya Sheria ya uendeshaji bunge kinaeleza ni nani anapaswa kuwa na jukumu la pale inapotokea mbunge amepata matatizo na kama sitaweza kujadili maslahi ya wabunge siyo Lissu peke yake ya wabunge wote akiwa ameumia au hajaumia Mhe. nipo tayari nisiwe mbunge, kama sisi ni wabunge hatuwezi kujadili maslahi ya wabunge? Huyu anasimama anaongea mzaa hapa tunaogea kuna mtu amepotea anaitwa Ben Sanane na kuna watu wanapotea na haya mambo yanahusu utawala bora, Katiba na Sheria na haya mambo ni ya msingi kuliko madaraja, lami haya mambo tukiyajaili kwa mioyo tunajenga msingi imara kwa sababu kuna watu wamepotea kuna mtu ameumia yupo hospitali na tunapojadili hatuwashtumu tunataka mrudi kwenye mstari, mjue tunajadili damu za watu"
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Vigezo na Masharti ya kufuatea wote wanakuwa na haki sawa Ndugai kafata vigezo na masharti huyu haini lafata mitandao na uamuzi WA familia na waliomzunguka karibunkama wewe. Wewe PIA zi ulipanda ndege bule kwenda nailoni?
    Je uamuzi na maadikuano yenu ealikuwa yepi?
    Je mlikuwa na mikakati gani huu ya malipo ya matibabu?
    Je hiyo ndege kea nini hamkiamua kumpeleka hsptl ya Rufaa falesalama muhimbili!
    Je Muhimbili waliku Ali au krsema hawana ujuzi na uwezo WA kimtibia huyu msaliti?
    Godilesi itapendeza kama utanuamaza na huh utumbu Wako.
    Bob Marley amekuharibu wakati WA zile sigara na sasa hufugi tens Lasta!!!..? Hukulukoni mwansngu...!!! Moe salami Baba Gambo kiboko yako.
    Usipayuke kea isiyo yajua...sigara zimekuwa adimu siku hizi Mwigulu kachoma shamba Zima umeipata!!!

    ReplyDelete
  2. Ahaaaaaa..... Dogo.... kama huna Mada au Hoja ya kuleta hapa Bungeni.
    Ningekuomba Uendeleee kutoka na Kama Bob Marley ndiyo kigezo chako. Basi ujue Misokoto imeanza kuwa Adimu, ajili Mwigulu ameshaanza kuchoma Mashamba.
    Na zile ulizo weka kwenye gari zimeshaanza kukauka na zinazidi ukali...!!!
    Rasta zako zimeishia wapi au kwa ajili ya Uheshimiwa?
    Uhuni haufaiiii.... Kuwa kiakili ili uwe Timamu.
    Sakozi yenu mmejaawatu wa dizaini yako..... Mkinyamaza Ntapendeza... manake hatuwaelewi wala hanjielewi.

    ReplyDelete

Top Post Ad