Mahesabu Aliyopiga Diamond Kumchukua Mbosso Yalikuwa Sahihi Asilimia 100....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


SIKU ZOTE KINACHOFANYA WATU KUSHINDA VITA SIO WINGI WA SILAHA BALI MBINU ZA UTUMIAJI WA SILAHA HIZO.

Nadhani Diamond Platnumz wakati anamchukua msanii Mboso na kumpa nafasi kwenye label yake yaWASAFI alishaona wazi kwamba huyu kijana ana hazina kubwa ya silaha ila huenda asingekuwa na mbinu nzuri ya kutumia silaha zake kwa mana hiyo mbali na silaha zake nyingi bado angeshindwa na watu wenye silaha chache.

Kitu kizuri kwa Diamondplatnumz ni kwamba yeye huwa siku zote ni baba katika kujua jinsi gani anazitumia silaha zake kuwamaliza maadui kwa mana hiyo kwa Mboso pia itakuwa rahisi sana.

#WATAKUBALI wimbo mpya wa Mbosso ni kama vile mtu kaenda kwenye vita halafu kabla vita havijaanza akarusha mshale kwanza kuwachokoza maadui zake ili wakiona mshale wajibu halafu ajue wana silaha gani ndio naye ashushe zile nzito alizo nazo.

#WATAKUBALI ni sawa kabisa na mshale tu kwa mana hiyo kuna MABOMU YA NUCLEAR ambayo kijana anasubiri kuona baada ya kutanguliza huo mshale watu watarudisha na silaha gani ili ndio aje kumaliza na mabomu mengine mazito.

Ninachokisema nadhani mtu aliyeenda kwenye utambulisho wa Mbosso juzi tarehe 28 pale HYATT atajua kabisa na maanisha nini juu ya huyu kijana Mbosso

Kitu ambacho Diamond Platnumz anafanikiwa sana ni kwa sababu hachukui mtu anayejua kuimba tu bali anachukua mtu mwenye kipaji cha vitu vingi ndio kama Mboso kijana ambaye anaweza kucheza na gita vizuri na huku anaimba live achilia mbali tungo zake zenye maandishi ya ki utu uzima.

WATAKUBALI huu ni mshale japo ni mshale wenye sumu ambao bado unaweza kumdhuru mtu mwenye bomu pale ambapo utampata.

HONGERA #WCB KWA KUENDELEA KUTOA NAFASI KWA VIJANA WENYE VIPAJI
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad