Maskini Mguu wa Mtoto Wanasa Kwenye Ngazi za Umeme Airport

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maskini Mguu wa Mtoto Wanasa Kwenye Ngazi za Umeme Airport
Mtoto Julian ambaye mguu wake ulinaswa kwenye ngazi za umeme kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver, Canada. Mama yake, Andrea Diaczok, ametoa wito kwa wazazi kuwa macho na watoto wao katika sehemu hizo.

MTOTO Julian mwenye umri wa miaka miwili alijikuta akivunjwa mifupa ya mguu wake uliponasa kwenye ngazi za umeme katika kiwanja cha ndege cha Vancouver, Canada.


Kiatu cha Julian kikiwa katika mashine za ngazi za umeme kilipokuwa kimenasa.

Julian alikuwa na wazazi wake, Andrea Diaczok, mama yake,  na baba yake, Jeff Lee walikuwa wakirejea mjini Calgary wiki iliyopita kutokea Vancouver.  Mguu wa mtoto huyo ulikwama pembeni kati ya ngazi na vyuma vinavyozungusha mikanda inayopandisha abiria.


Julian akiwa amelazwa hospitali akipatiwa matibabu, kinyume na woga wa wazazi wake ambao walifikiri huenda mguu wake ungekatwa.

“Mguu wake ulipotea kabisa kwenye mkanda unaozunguka,” Diaczok, alisema na kuongeza kwamba kuona hivyo alipiga kelele kwa nguvu.


Wazazi wa Julian wakifurahi naye baada ya matibabu ya mguu wake ambayo yalichukua wiki kadhaa.

“Mtambo huo uliukunja mguu wake na kuvunja mifupa ya mguu ambapo kiatu chake kilipotelea ndani ya mkanda huo wenye kuzunguka,” alisema.

Kiatu cha Julian kilikuwa kimebanwa kwenye mkanda huo na ilibidi wafanyakazi wa uwanjani hapo na wapita njia kumng’oa mahali hapo aliponasa.

Diaczok na Lee ambao ni wafanyakazi katika fani ya afya, walikuwa wamejitayarisha kwamba mwanao angekatwa mguu. Hata hivyo, madhara hayakuwa makubwa sana, kwani mbali na mifupa iliyokuwa imevunjika na miteguko kadhaa, madaktari waliweza kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu ambayo hayakuwalazimisha kuukata mguu huo.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad