Serikali Kuimarisha Mifumo ya Utoaji Huduma za Dawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Serikali Kuimarisha Mifumo ya Utoaji Huduma za Dawa
SERIKALI imesisitiza kwamba itaendelea kuimarisha mifumo yake ya utoaji huduma za dawa kutokana na ukweli kwamba ya dawa zinatumika kwa wanyama na binadamu na kuleta usugu wa ugonjwa
husika kwa mgonjwa na gharama kubwa kwa taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dr Faustine Ndugulile wakati wa Ufunguzi wa mkutano wa Kimataifa wa siku nne wa Jukwaa la kudhibiti usambazaji na uzalishaji wa bidhaa za madawa Afrika ambapo nchi 18 zipo nchini kujadili namna bora ya kudhibiti madawa yasiyo na viwango katika soko ili kuimarisha na ustawisha afya za wananchi wake.

“Tanzania ni moja ya nchini iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa katika udhibiti wa dawa feki kwa Afrika nzima na mamlaka ya dawa na vipodozi nchini ina maabara za kisasa na watalaamu wa kutosha wa kuweza kufanya ukaguzi wenye ubora na viwango vya kimataifa,” amesema Ndungulile.

Ameongeza kwamba Tanzania imeweza kujitosheleza kwa dawa za kutosha na zenye viwango vya kimataifa na changamoto kubwa ilikuwa  kudhibiti dawa zinazoingia kwa njia ya panya ambapo tayari mamlaka husika wameshafungua ofisi za kanda ambazo zimefanya kazi kubwa kupunguza mianya ya dawa zinazoingia kwa njia ya panya.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bi Agnes Kijo amefafanua kwamba wataalamu kutoka nchi za Cameron, Ivori Coasti, Mali, Nigeria, Ghana, Burkina Faso, Mauritius, Senegal, Ethiopia, Sudan, Guinea, Sierra Leone, Uganda, Malawi, Zambia, Zimbabwe na Afrika kusini watakutana kwa siku nne ili kuja na mpango kabambe wa kudhibiti dawa bandia.

“katika mkutano huu jambo kuu litakuwa na kwa namna ngani tunaweza kudhibiti dawa bandia kwenye masoko na kuhakikisha kwamba wazalishaji pia wanatoa dawa zenye ubora unaokubalika katika soko,”
amesema  Kijo.

Kijo ameongeza kwamba TFDA kwa sasa ina maabara 24 nchi nzima zenye vifaa vya kisasa vya kufanya ukaguzi
nchini nzima na ofisi saba za kikanda ambazo zina wataalamu wa kutosha kuweza  kuhudumia sehemu za mikoani.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad