Trump Ampiga Stop Diego Maradona Kuingia Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Trump Ampiga Stop Diego Maradona Kuingia Marekani
Rais wa Marekani Donald Trump ameripotiwa kumpiga marufuku mchezaji wa zamani wa Argentina na mshindi wa Kombe la Dunia, Diego Maradona kuingia nchini Marekani.


Mwanasheria wa mwanasoka huyo wa zamani amesema kuwa Maradona hatohudhuria kesi yake jijini Miami kutokana na nyota huyo kuzuiwa na Rais Trump kwa madai kuwa alitoa lugha ya kashfa kwa Trump kwenye mahojiano na Television nchini Venezuela.

''Maradona hatoweza kuwepo kwenye kesi yake dhidi ya mke wake wa zamani kwasababu amezuiwa na Rais Trump'', amesema Mwanasheria huyo.

Muargentina huyo alihitajika kusafiri wiki hii kwenda Miami, Florida, kwenye kesi yake dhidi ya mke wake wa zamani Claudia Villafane, ambaye anamshitaki kwa kumuibia fedha na kununua mali mbalimbali nchini Marekani.

Maradona anakumbukwa kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani, akiwa nahodha wa Argentina alirudishwa nyumbani baada ya kupimwa na kugundulika ametumia madawa ya kulevya aina ya Cocaine.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad