Trump Awatoa Hofu Wafuasi Wake Amchimba Mkwara Oprah

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Trump Awatoa Hofu Wafuasi Wake Amchimba Mkwara Oprah
Rais wa Marekani, Donald Trump amewatoa hofu wafuasi wake  baada ya tetesi kuwa huenda mwanamke Mjasiriamali, Oprah Winfrey atajitupa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa nchi hiyo mwaka 2020.

Trump amesema anamfahamu sana Mwanamama huyo na ni moja ya watu ambao huwa anafuatilia viindi vyake ingawaje huwa anaboreka na namna ya uuliza maswali yake kwa wageni anaowaalika kwenye show zake huku akipindisha baadhi ya ukweli wa mambo.

“Nimemtazama Oprah Winfrey mtu asiyekuwa madhubuti, ambaye kwa upande mmoja namfahamu vizuri, nimekuwa nikimtazama akifanya mahojiano na watu wengi kwa dakika 60. Maswali yake yamekuwa ya upendeleo, yamekosa mwelekeo na amekuwa akipindisha ukweli, natumaini Oprah anaweza akajitokeza na kugombea urais na nitamshinda kama nilivyowafanyia wenzake,“ameandika Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Mwishoni mwa mwaka jana Oprah wakati akitoa hotuba yake katika ugawaji wa tuzo za Golden Globe aliushitua ulimwengu baada ya kutangaza kuwa  anaweza akagombea Urais wa Marekani mwaka 2020.

Hata hivyo, baadaye Oprah kupitia kipindi chake cha ‘Daytime Talk Show’  alikuja kukanusha uvumi huo kwa kusema kuwa alitania tu ili kunogesha hotuba kwani kazi hiyo haipo kwenye damu yake.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad