Yanga Kibaluani Kesho Kuumana na Shelisheli St Louis

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Kibaruani Kesho Kuumana na Shelisheli St Louis
Klabu ya soka ya Yanga inatarajiwa kushuka Dimbani Kesho Jumamosi kuumana na Mabingwa wa Shelisheli St Louis, lakini kikosi hicho kitawakosa nyota wake wanne wa kikosi cha kwanza.

Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa ya Daktari wa timu hiyo Edward Bavu imeonesha kuwa wachezaji Donald Ngoma, Abdalah Shaibu, Yahana Nkomola na Amiss Tambwe hawatakuwa sehemu ya mchezo huo.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema, mchezo wa kesho ni muhimu kwa timu yake na kwani utaisaidia Yanga kufikia malengo yake katika michuano ya kimataifa.

Kwa upande wake kocha mkuu wa St Louis ya Shelisheli Michel Renald amesema wamekuja kucheza na yanga na wanaiheshimu na mchezo wa kesho watahakikisha wanautumia vyema kupata matokeoyatakayowawezesha kusonga mbele katika ligi ya Mabingwa.

Yanga inatarajiwa kutupa karata yake ya kwanza katika michuano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa kuumana na mambingwa wa Shelisheli St Louis katika mchezo unatarajiwa kupigwa katika dimba la Uhuru Jijini Dar es salaam.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad