Waziri Mwigulu Ata Agiza kwa Jeshi la Polisi Kuziachia Pikipiki Zinazoshikilia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Mwigulu Aagiza Kuachiwa Pikipiki Zinazoshikiliwa na Jeshi la Polisi
February 9, 2018 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dr. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuziachia pikipiki ambazo wamezishikilia kwa muda mrefu na zina makosa madogo na kwamba wasikae nazo kwa muda mrefu mpaka zikawa vyuma chakavu.

Dr. Mwigulu amesema zile yenye makosa makubwa kama uhalifu wa kivita, dawa ya kulevya wabaki nazo na wafanye utaratibu wa kuwapeleka Mahakamani au kuziteketeza na zenye makosa madogo wazirudishe kwa wamiliki na kuwapa elimu wamekosea wapi.

“Wapeni masomo wamekosea wapi, waelekezeni na waliowabishi warekebisheni lakini tusirundike tukatengeza vyuma chakavu kwa hivi vitu ambavyo utatuzi wake tunao, tutumie huu mkono kwa kutatua yale ambayo yapo ndani ya mamlaka yetu” – Dr Mwigulu

Amesema kuwa ipo haja sasa vijana kufundishwa zaidi kuhusu sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za pikipiki na mlundikano wa pikipiki katika vituo vya polisi nchini kwani kila anapopita katika vituo vya polisi hukuta pikipiki nyingi na makosa yao ni madogomadogo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad