Zitto Kabwe Amtembelea Samatta Nyumbani Kwake Ubelgiji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zitto Kabwe Amtembelea Samatta Nyumbani Kwake Ubelgiji
Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa jana jioni alikwenda Genk nchini Ubelgiji nyumbani kwa nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta.

Zitto amesema kuwa amefurahi kumsalimia na kumjulia hali Samatta huku akieleza kuwa amefurahi kumkuta akiwa mzima wa afya.

Nimepita Kumsabahi Nahodha Samatta – Zitto

Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji.

Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi.

Namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Genk
Ubelgiji
Februari 13, 2018
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad